|
Mwanafunzi mwenye
ulemavu (kushoto) wa Shule ya Msingi Nguvumali akiwa anafurahia maziwa huku
akimwangalia mwanafunzi mwenzake mara baada ya kupatiwa maziwa kutoka Bodi ya
Maziwa nchini (TDB) ikiwa ni siku ya kwanza ya maadhimisho ya wiki ya unywaji
maziwa kitaifa yanayofanyika Mkoani Tanga. (Picha
na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi) |
|
Mwanafunzi wa Shule
ya Msingi Nguvumali Samira Shaban akipatiwa maziwa na mwalimu wake, mara baada
ya maafisa kutoka Bodi ya Maziwa nchini (TDB) na Mkoa Tanga, kufika katika shule
hiyo kwa lengo la kuhamasisha unywaji maziwa kwa watoto ili kuimarisha afya zao
ikiwa ni moja ya shughuli ambazo bodi hiyo itakuwa inafanya katika maadhimisho ya
wiki ya unywaji maziwa kitaifa yanayofanyika Mkoani Tanga kwa kuyafikia makundi
ya watu wenye mahitaji maalum. (Picha na Edward
Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi) |
|
Mmoja wa walimu wa
lugha ya alama katika Shule ya Msingi Chuda, akitoa tafsiri kwa wanafunzi wenye
ulemavu wa kutosikia mara baada ya maafisa kutoka Bodi ya Maziwa nchini (TDB)
na Mkoa wa Tanga kufika katika shule hiyo, kwa lengo la kuhamasisha unywaji maziwa
kwa watoto ili kuimarisha afya zao ikiwa ni moja ya shughuli ambazo bodi hiyo
itakuwa inafanya katika maadhimisho ya wiki ya unywaji maziwa kitaifa
yanayofanyika Mkoani Tanga kwa kuyafikia makundi ya watu wenye mahitaji maalum.
(Picha na Edward Kondela, Afisa Habari –
Wizara ya Mifugo na Uvuvi). |
|
Kaimu Afisa Lishe Mkoa wa Tanga Bi. Sakina Mustapha,
akiwafahamisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Nguvumali umuhimu wa unywaji maziwa,
mara baada ya Bodi ya Maziwa nchini (TDB) kugawa maziwa kwa wanafunzi wakiwemo
wenye mahitaji maalum katika shule za msingi Usagara, Chuda na Nguvumali katika
siku ya kwanza ya maadhimisho ya wiki ya unywaji maziwa kitaifa yanayofanyika
Mkoani Tanga kuanzia Tarehe 31 Mei hadi 04 Juni 2021. (Picha
na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi). |
|
Afisa Msindikaji wa Maziwa kutoka Bodi ya Maziwa
nchini (TDB) Bw. Dotto Nkuba, akizungumza mara baada ya kuhitimisha zoezi la
ugawaji maziwa kwa shule za msingi Usagara, Chuda na Nguvumali katika siku ya
kwanza ya maadhimisho ya wiki ya unywaji maziwa kitaifa yanayofanyika Mkoani
Tanga na kufafanua kuwa bodi hiyo itaendelea kuyafikia makundi mbalimbali ya
watu wenye mahitaji maalum katika kuhamasisha unywaji maziwa ili kuimarisha
afya ya mwili. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari
– Wizara ya Mifugo na Uvuvi). |
Picha
ya pamoja ya maafisa kutoka Bodi ya Maziwa nchini (TDB), Mkoa wa Tanga na
baadhi ya walimu na wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi
Usagara baada ya wanafunzi hao kupatiwa maziwa na bodi hiyo katika siku ya kwanza
ya maadhimisho ya wiki ya unywaji maziwa kitaifa yanayofanyika Mkoani Tanga. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari –
Wizara ya Mifugo na Uvuvi).Na. Edward Kondela
Bodi ya
Maziwa nchini (TDB) imesema katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora
imeamua kugawa maziwa kwa watu wenye mahitaji maalum kutokana na virutubisho
vilivyopo kwenye maziwa hayo ambavyo vitawasaidia kuimarisha afya zao.
Akizungumza
leo (31.05.2021) mara baada ya kuhitimisha siku ya kwanza ya ugawaji maziwa
ikiwa ni sehemu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na TDB katika maadhimisho
ya wiki ya unywaji maziwa kitaifa yanayofanyika Mkoani Tanga, kuanzia tarehe 31
Mei hadi 04 Juni Mwaka 2021, Afisa Msindikaji wa Maziwa kutoka bodi hiyo Bw. Dotto
Nkuba amesema katika siku ya kwanza bodi imetembelea shule tatu za msingi za
Mkoa wa Tanga ambazo pia zinawahudumia watoto wenye mahitaji maalum ili kutoa
kipaumbele kwa watoto hao kunywa maziwa na kuhamasisha jamii kuwa na utaratibu
kwa kunywa maziwa ili kuimarisha afya zao.
“Lengo
la kutoa maziwa kwa watu wenye mahitaji maalum tunahimiza kunywa maziwa kutokana
na virutubisho vitokanavyo katika maziwa na tumeangalia watoto wa shule kwa
siku ya leo na hii haimaanishi watu wengine wasinywe maziwa bali wanywe kwa
faida ya afya zao ila hatua hii itakuwa mwendelezo wa kuyafikia makundi mengine.” Amesema Bw.
Nkuba
Ameongeza kuwa
maadhimisho ya wiki ya unywaji maziwa kitaifa yanayofanyika Mkoani Tanga,
yanalenga kuhamasisha wananchi kunywa maziwa kwa sababu ni chakula ambacho kina
virutubisho vyote ambavyo ni muhimu kwa mwili wa binadamu hususan maziwa
yaliyosindikwa ambayo yamekidhi ubora.
Aidha,
amesema Bodi ya Maziwa nchini inahimiza wananchi kunywa maziwa kwa wingi ili
kuwa na utamaduni wa kunywa maziwa na kuviwezesha viwanda vya kuchakata maziwa
nchini kuuza bidhaa zao kwa wingi.
Kwa upande
wake Kaimu Afisa Lishe Mkoa wa Tanga Bi. Sakina Mustapha, amesema wamekuwa
wakifanya kazi kubwa ya kutoa elimu juu ya umuhimu wa unywaji maziwa kutokana
na maziwa kuwa na madini na vitamini pamoja na maji ambavyo vyote hivyo
vinajenga mwili, kulinda mwili, kuongeza ufanisi wa kujenga mifupa sambamba na
meno, kupata sukari na nguvu mwilini pamoja na nguvu ya ziada ya kufanya kazi.
Bi.
Mustapha amewaasa wananachi kwa ujumla kunywa maziwa walau kikombe kimoja kila
siku ili kuuwezesha mwili kuongeza virutubisho muhimu vitokanavyo na maziwa.
Wanafunzi
waliopatiwa maziwa leo na Bodi ya Maziwa nchini ni kutoka katika Shule za
Msingi Chuda, Nguvumali na Usagara zilizopo jijini Tanga na zoezi la ugawaji
litaendelea kwa kuyafikia makundi mbalimbali ya watu maalum.
Maadhimisho
ya wiki ya unywaji maziwa kitaifa yanafanyika Mkoani Tanga kuanzia Tarehe 31 Mei
hadi 04 Juni Mwaka 2021, katika viwanja vya Tangamano yakiwa yamebeba kauli
mbiu “Kunywa Maziwa ya Kwetu, Ongeza
Uzalishaji na Usindikaji, Kazi Iendelee.”
Post A Comment: