_Hadi sasa chasafisha kilo 63.1_


Na Samweli Shoo, Tume ya Madini


Imeelezwa kuwa tangu kuanzishwa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Mwanza, jumla ya kilo 63.179 zimesafishwa kwa ubora wa  asilimia 99.99.


Hayo yameelezwa leo tarehe 27 Mei, 2021  na mtaalam kutoka katika kiwanda hicho, Deusdedith Magala kwenye ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula na Kamishna wa Tume ya Madini, Janeth Lekashingo waliyoifanya katika kiwanda hicho kilichopo Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.


Kiwanda hicho kinamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)na mwekezaji kutoka Dubai.


Mara baada ya kupata maelezo kutoka katika Kiwanda hicho, Profesa Kikula alipongeza utendaji wa kiwanda hicho na kuwataka watendaji wake kuendelea kuchapa kazi kwa bidii


Katika hatua nyingine viongozi hao wa Tume wametembelea Ofisi ya Madini na soko la Madini Mwanza ambapo wametoa pongezi kwa watumishi wa Ofisi ya Madini  Mwanza kwa kuvuka lengo la makusanyo ya maduhuli  kwa  asilimia152 katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: