Meneja wa Kampuni ya Uchimbaji  Dhahabu ya Shanta Mradi wa Mkoa wa Singida, Jiten Divecha (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo moja ya dawati kati ya 183 yaliyotolewa na kampuni kwa Shule ya Sekondari ya Mang'onyi Shanta katika hafla iliyofanyika jana wilayani humo. Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Mang'onyi, Innocent Makomelo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza wakati wa hafla ya kupokea madawati hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Jusitce Kijazi, akizungumza kenye hafla hiyo.

Meneja wa Kampuni ya Uchimbaji  Dhahabu ya Shanta Mradi wa Mkoa wa Singida, Jiten Divecha, akitoa taarifa fupi ya msaada huo.

Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Elisante Kanuya akizungumza katika hafla hiyo.
Wananchi na viongozi wa kata hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Kaimu Afisa Tarafa ya Ikungi, Yahaya Njiku akizungumza katika hafla hiyo.

Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Ikungi, Margaret Kapelesya, akizungumza katika  hafla hiyo.

Mkuu wa Shule hiyo,  Frorence Rwaigemu akisoma taarifa ya shule kabla ya  kukabidhiwa madawati hayo.

Majadiliano na mkuu wa wilaya yakifanyika wakati wa hafla ya kupokea madawati  hayo.

Hafla hiyo ikiendelea. Kushoto ni Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Ikungi, Margaret  Kapelesya akiwa na Mratibu wa Afya na Lishe Shuleni wilayani humo, Prisca Masenga.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.

Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.

Hafla ikiendelea.
Makabidhiano ya madawati hayo yakifanyika.

Wanafunzi wa shule hiyo wakiyatizama madawati waliyokabidhiwa na kampuni hiyo ya Shanta.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mang'onyi, Stanley Shabani akizungumza kwenye hafla hiyo.

Meneja wa Kampuni ya Uchimbaji  Dhahabu ya Shanta Mradi wa Mkoa wa Singida, Jiten Divecha (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ikungi baada ya kukabidhi madawati hayo. Kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Elisante Kanuya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi.na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo.

Viongozi wa Kata ya Mang'onyi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumpokea madawati hayo. kulia ni Diwani wa hiyo, Innocent Makomelo. 


Na Waandishi Wetu, Singida


KAMPUNI ya uchimbaji dhahabu ya Shanta-mradi wa Singida imekabidhi msaada wa madawati 183, sambamba na kukarabati madarasa 5 ya shule ya Sekondari Mang'onyi, iliyopo wilaya ya Ikungi mkoani hapa.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo jana, mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo,  Meneja wa Shanta kwa mradi wa Singida, Jiten Divecha alisema mpango huo unalenga kusaidiana na serikali katika kuboresha mazingira ya kujisomea kwenye shule mbalimbali ndani ya mkoa huo.

"Madhumuni ya mchango wetu huu ambao umegharimu jumla ya shilingi milioni 22.5 ni kuhakikisha wanafunzi wapya waliosajiliwa kuingia kidato cha kwanza na waliopo wanakuwa na mazingira bora ya kusomea," alisema Divecha.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo Mpogolo, kwa niaba ya serikali ya Awamu ya Sita alipongeza na kushukuru uongozi wa Shanta kwa hatua hiyo muhimu ya mahusiano ambayo inaashiria mwanga mzuri, ustawi na ukuaji wa pamoja kwa maendeleo.

"Napongeza hatua hii ambayo imefanyika katika kipindi ambacho Shanta ipo kwenye ujenzi na utafiti wa mgodi wao kabla ya kuuzindua rasmi," alisema Mpogolo.

Zaidi, aliwaagiza watendaji ndani ya sekta ya elimu kuhakikisha wanaweka usimamizi mzuri wa utunzaji wa vifaa na miundombinu iliyotolewa ili kutoa fursa ya watoto kupata elimu bora, sanjari na kuongeza hamasa ya walimu kufundisha.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya alitumia hafla hiyo kuhamasisha watendaji juu ya umuhimu wa kuimarisha mahusiano na wawekezaji ili kuharakisha maendeleo na ustawi wa watu.

"Tukitunza madawati na madarasa haya ni dhahiri watoto watasoma vizuri, baadaye wataajiriwa ndani ya mgodi huu...na wengine watakuwa viongozi wa taifa letu kwa ustawi wa wanamang'onyi, Singida na Tanzania kwa ujumla," alisema Mpogolo na kuongeza;

"Pia mahusiano mazuri na mwekezaji yatatusaidia hata kukusanya vizuri mapato ya serikali kutoka kwa Shanta wenyewe na wazabuni wao wote watakaoshirikiana nao," alisema.

Share To:

Post A Comment: