Hayo yamesemwa na katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii amabye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo Dkt Allan Kijazi ambapo amemwakilisha Waziri wa wizara hiyo Dkt Damas Ndumbaro, katika ufunguzi wa mkutano wa 28 wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na utalii uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Arusha, Kijazi amewataka watumishi kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kufikia malengo yaliyowekwa.
Na Lucas Myovela _ Arusha.
Ukiwa ni ufunguzi wa mkutano 28 wa Baraza hilo ambapo Dkt Kijazi ameweza kuongea na watumishi mbali mbali wa wizara hiyo pamoja na taasisi za umma amesema kuwa suala la ukusanyaji wa maduhuli ni suala muhimu kwa wizara kama inavyoelekezwa katika sheria,kanuni na miongozo mbalimbali ya serikali.
Dkt Kijazi asema watumishi wanapaswa kukuza wigo wa bidhaa za utalii ili kufikia watalii milioni 5 na kuongeza mapato hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 6 ifikapo mwaka 2025, ili kufikia azma hiyo wanapaswa kuimarisha utalii wa uwindaji wanyama pori, kukuza utalii wa mikutano pamoja na kuendeleza utalii wa fukwe.
"Katika hazma ya kufikia malengo haya mnapaswa kuimarisha usimamizi, ulinzi na uhifadhi wa maliasili kwa faida yakizazi cha sasa na kizazi kijacho kwa kuendelea kujenga uwezo wa wadau katika kusimamia rasilimali za wanyapori,misitu na nyuki pamoja na kuendelea kudhibitib ujangili wa wanyama pori na mazao ya misitu na nyuki kwa kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia uwekezaji katika sekta ya utalii". Amesema Kijazi
“Lakini pia tunatakiwa kuendelea kusimamia, kuendeleza na kulinda mali kale kwa manufaa ya taifa kwa kuboresha usimamizi, matumizi na uhifadhi wa maeneo ya malikale na urithi wa utamaduni ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu wezeshi ya utalii katika maeneo hayo kwa kuweka mazingira ya kuvutia wawekezaji na kuhamasisha kufanyika kwa matamasha ya kitamaduni,” Alisema Dkt Kijazi.
Aidhsa Dkt Kijazi, ameeleza kuwa serikali kwasasa inatoa kipaumbele katika kuboresha maslahi ya watumishi ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya msingi kwa ufanisi na serikali imetoa kibali cha kuwapandisha vyeo watumishi wenye utendaji mzuri na waliotengewa nafasi katika mwaka wa fedha 2018/2019 na 2020/2021.
“ Nina agiza wizara na wakuu wa Taasisis zote zilizo chini ya wizara ya maliasili na utalii kuwapandisha vyeo kabla ya Mei 31 watumishi wote wanaostahili pamoja na kuendelea kuwapa mafunzo ya muda mfupi na mrefu ili kuweza kuwajengea uwezo na weledi utakao wawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi unaotarajiwa". Aliongeza Dkt Kijazi.
“Pia ninawaomba muendelee kuimarisha nidhamu, ukakamavu na uadilifu katika kutekeleza majukumu yenu ya uhifadhi na nimatumaini yangu kuwa matukio ya ujangili na biashara haramu ya mazao ya wanyapori na misitu yatapungua kwa kiasi kikubwa kutokana na jitihada zinazoendelea kufanya na Jeshi letu la uhifadhi wanyama pori na misitu,” Alisema Kijazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya utawala na rasilimali watu Bw Lucius Mwenda,ameeleza kuwa wao wameyachulua yote yaliyo elezwa na yatawasaidia kujua mwajiri anataka nini na ni nini kimepangwa na wao watahusika katika kutekeleza ambapo kwa asilimia.
Naye mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi {TUGHE} tawi la maliasili na utalii Antony Tibaijuka alieleza kuwa wamepewa nafasi ya kupitia bajeti pamoja na kupewa ruhusa ya kuzunguza yale waliyonayo jambo ambalo litawafanya wafanyakazi kutekelezamajukumu yao vizuri na kufikia malengo yanayo hitajika.
Post A Comment: