Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amepongeza juhudi zinazofanywa na Wauguzi katika utoaji bora wa huduma za afya.

Muro amesema  hayo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

Amesema,Serikali imeboresha miundombinu  katika sekta ya Afya kwa kujenga Hospitali ,vituo vya afya pamoja na kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa dawa ambapo Wauguzi wanawajibu mkubwa kuchochea maendeleo hayo kwa hutoaji wa huduma bora.

Muro ametoa Wito kwa Wauguzi  kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi mkubwa "Serikali imeahidi kushughulikia stahiki za watumishi ,natoa rai kwenu kuchapa  kazi kwa maendeleo ya Taifa"amehimiza Muro

Aidha Muro amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanalipwa stahiki za watumishi ambazo hazina ulazima wa kusubiri.

Ikumbukwe leo ni maadhimisho ya siku ya Wauguzi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: