Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida Dkt. Denis Nyiraha 


Na Dotto Mwaibale


MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM) Mkoa wa  Singida,  Dkt. Denis Nyiraha amesema Katibu Mkuu wa chama hicho aliyechaguliwa juzi Daniel Chongolo na Katibu wa Itikadi na Siasa, Shaka H.Shaka kuwa ni viongozi ambao watakidhi kiu ya wana CCM na wananchi kwa ujumla.

Nyiraha aliyasema hayo juzi baada ya kumalizika kwa  mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Dodoma.

" Viongozi hawa ni wazoefu katika chama chetu na kazi zao zilikuwa zikionekana kwa kukitumikia chama chetu na Serikali hivyo kuchaguliwa kwao kutakidhi kiu za wananchi." alisema Nyiraha.

 Dkt. Nyiraha alisema kuwa viongozi hao watashusha kiu ya wananchi katika majukumu yao ya kila siku na kuongeza ari ya utendaji kwa kuwa wanauzoefu na uwezo na kuwa wamekuja wakati sahihi.

Nyiraha amewahikishia wananchi  kuwa chama kimepata viongozi sahihi chini ya Mwenyekiti wao wa Taifa Rais Samia Suluhu Hassan na akaomba wapewe ushirikiano.

Share To:

Post A Comment: