Naibu Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Richard Kangalawe amesema maonesho ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ni muhimu sana  kwa sababu wanaoshiriki Maonesho wanaona bunifu ambazo taasisi zimeandaa, wanajionea programu zinazoendeshwa na Vyuo husika na pia wanapata fursa ya kujifunza



Prof Kangalawe amesema  miongoni mwa majukumu ya   Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni pamoja na kufundisha, kufanya tafiti, kuchapisha na kuandaa bunifu mbalimbali ambazo zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili Jamii.

“ Ninawataka Wanafunzi wabunifu kuendelea kubuni ili kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili Jamii, mfano Mlemavu hawezi kuongea lkn akitumia kifaa kilichobuniwa ambacho ni Fimbo Maalumu maana yake kitamsaidia  kujielekeza wenyewe,” alisema Prof. Kangalawe.

Maonesho haya yamefunguliwa  leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa yatahitimishwa Juni 2, 2021.


Imeandaliwa na:

KITENGO CHA HABARI NA MAHUSIANO- 

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

Share To:

msumbanews

Post A Comment: