Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) leo alfajiri Mei 8, 2021 imezindua rasmi safari za ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou nchini China.
Uzinduzi huo uliofanyika kwenye Jengo Namba 3 la abiria (terminal 3) katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere umeongozwa na Mhandisi. Dkt. Leonard Chamuriho, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi. Ladislaus Matindi.
Kwa mujibu wa ATCL, safari kati ya Dar es Salaam na Guangzhou itatumia saa 11 na zitakuwa safari pekee za moja za moja kwa moja kati ya maeneo hayo mawili.
Tangu mwaka 2015 serikali imewekeza nguvu katika kufufua kampuni hiyo ambapo jitihada hizo ni pamoja na kununua ndege, kukarabati na kujenga viwanja vya ndege na kuongeza rada za kuongozea ndege ili kuziwezesha ndege za shirika hilo kufika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Post A Comment: