Mkurugenzi wa Zahanati ya Manundu Dkt Ali Mzige akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani

Dkt Ali Mzige akiwaonesha waandishi wa habari bango lililoandikwa madhara mbalimbali ya matuminzi mabaya ya chakula

 

WITO umetolewa kwa wakina mama wajawazito wanaopendelea kula chips mayai wakati wa mimba kuacha  kwani kuendelea kutumia kuna uwezekano mkubwa wa kupata kisukari cha mimba

Hayo yalisemwa Mkurugenzi wa Zahanati ya Manundu, Dkt Ali Mzige katika Kongamano la afya lililokuwa na kauli mbiu ‘Pima afya yako kabla hujaugua,’ambapo aliwataka wakina mama wajawazito kuwa makini na aina ya vyakula wanavyotumia.

Dkt Mzige aliwashauri pia wakina mama wanaotengeneza unga wa lishe kwa ajili ya watoto kwamba unga huo una aina nyingi za nafasi hivyo haufai kwa matumizi ya watoto.

“Nitoe wito kwa wakina mama wajawazito wanaopendelea kula chips mayai wakati wa mimba kuacha kwani matumizi ya chakula hicho upo uwezekano wa kupata kisukari cha mimba”Alisema

Pia alishauri akina mama wanaotengeneza unga wa lishe kwa ajili ya watoto kwamba unga huo uliokuwa na aina nyingi za nafaka haufai kwa matumizi ya watoto.

Hata hivyo Dkt Mzige alisema pia Ulaji mbaya wa chakula, usiozingatia kanuni za kiafya, unaweza kuchangia magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu na hivyo imeshauriwa watu wabadili taratibu za mlo kila siku.

Dkt Mzige ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Kinga na Tiba wa Wizara ya Afya, alisema magonjwa mengi kama kisukari, shinikizo la damu na saratani husababishwa na watu kutozingatia kanuni za chakula wanachokula.

Akashauri watu wapunguze nishati lishe za ziada (extra calories) matumizi ya sukari, mafuta yenye lehemu (cholesterol) na chumvi.

Aidha aliwataka watumie vyakula vya asilia vyenye lishe makapi-fibre, kula dona badala ya sembe nyeupe, mihogo, magimbi, viazi vitamu vikipikwa kwa kuchemshwa bila kukaangwa ni bora kuliko chips.

Hata hivyo Dkt Mzige katika mkutano wake na waandishi wa habari alitumia nafasi hiyo kutambulisha kituo chake kipya cha Mshangai Preventive Medical Care Polyclinic, itakayokuwa na jopo la madaktari bingwa watatoa huduma zote za magonjwa yanayotokana na matatizo mbalimbali ikiwemo saratani.

 

Mwisho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: