Jafary  Kachenje Mkaguzi mkuu wa ndani waWizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki akizungumza na waandishi jijini Arusha.

Na Lucas Myovela, Arusha

WAKAGUZI  ndani bara la Afrika wamekutana jijini Arusha kujadili matumizi ya teknolojia katika utendaji kazi itakayowawezesha kuboresha ukaguzi wao kwa kupitia teknolojia.

Akifungua mkutano wa 7 wa wakaguzi wa ndani wa Afrika (AFIIA) Mwenyekiti wa Taasisi ya wakaguzi hao Emmanuel Johanes alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuleta manufaa katika uchumi wa nchi za Afrika.

Johanes alisema kuwa  pia wataweza kujadili matatizo  mbalimbali ya wakaguzi na kujua jinsi ya kusaidia kuchangia maendeleo ya nchi za Afrika pamoja na suala zima la kuboresha uwezo wa wakaguzi na kujifunza kutoka nchi zingine.

“Hapa tutabadilishana uzoefu kila mmoja atajua nchi nyingine wanafanya nini na ni namna gani na sisi tunaweza kuboresha mikakati mbalimbali ya kupiga hatua katika maendeleo ya kiuchumi.”Alisema Johanes

Alifafanua kuwa yapo matatizo  mbalimbali ya kiutandaji,uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi pamoja na uhaba  wa bajeti za kuwezesha kazi kufanyika ambapo katika sekta ya umma bado wakaguzi wana shida nyingi kutokana na kutokuwa na bajeti na vifaa pamoja na mafunzo ya kutosha.

Kwa upande wake Jafary Kachenje Mkaguzi mkuu wa ndani wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki alisema kuwa ili kuweza kuepuka matatizo  ambayo hutokea mara kwa mara,mafunzo ambayo wakaguzi wa ndani hupatiwa yanapaswa kutolewa kwa wakurugenzi na kwa kufanya hivyo yatawasaidia kufahamu umuhimu wa wakaguzi wa ndani katika taasisi zao.



Kwa upande wake  mkaguzi Mkuu wa ndani wa benki ya CRDB nchini Burundi Aloyce Leonard amesema wakaguzi wanatakiwa kuwa na uwezo wa kutoa uhakiki katika taasisi kulingana na mabadiliko ya teknolojia yanavyokwenda na kuendana na teknolojia mpya  ambapo mkutano huu wa 7 unafanyika jijini Arusha kwa siku nne na umejumuisha mataifa mbalimbali barani Afrika ikiwemo nchi ya Tanzania.
Share To:

Post A Comment: