Na Farida Saidy, MOROGORO.
KATIKA kuboresha na kuimarisha huduma za uokoaji kwa lengo la kuondoa malalamiko ya Wananchi wakati wa majanga mbalimbali Nchini, Jeshi la zimamoto na Uokoaji limeanza kutekeleza makubaliano kati ya Jeshi hilo na chama cha Skauti juu ya kushirikiana katika majukumu kwa kuanza kutoa mafunzo ya awali ya zima moto na uokoaji kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari.
Hayo yameelezwa na Kamishna wa Jeshi la zimamoto na ukoaji John Masunga kwenye kikao kazi cha Baraza dogo la Wafanyakazi wa Jeshi hilo kwa ajili ya kupokea taarifa ya Bajeti ya Mwaka 2020 na mwelekeo wa fedha wa 2021.
Akizungumza katika kikao hicho Kamishna wa Jeshi la zimamoto na ukoaji amesema,Jeshi hilo limejipanga kuhakikisha linamaliza malalamiko ya Wananchi wakati kunapotokea majanga mbalimbali katika maeneo kwa kuboresha huduma za uokoaji.
“Nataka niwambie sisi kama Jeshi la zima moto tunatalajia ifikapo mwaka 2023 tutakuwa tumefika wilaya zote za Tanzania Bara ili kuhimarisha huduma za uokoaji kwa Wananchi”.Alisema Kamishna wa Jeshi la zimamoto na ukoaji John Masunga.
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Skauti Wilaya ya Morogoro Bwana Frank Kaundula ameeleza namna watakavyo shirikiana na Jeshi la zimamoto na uokoaji inapo tokea majanga mabalimbali katika mane ohayo.
“Kama wilaya tumeshaanza kutengeneza makundi maalumu ya vijana wa Skauti kutoka katika shule za Sekondari na Msingi watakaopatiwa mafunzo maalumu ya uokoaji kutoka kwa Askali ya zimamoto na uokoaji.”Alisema Naibu Kamishna wa Skauti Wilaya ya Morogoro Bwana Frank Kaundula
Hata hivyo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bwana Emmanuel Kayui amewataka Askari wa Jeshi la zimamoto na uokoaji kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia sharia.
Post A Comment: