Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,akizungumza wakati akifunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato,akizungumza na Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akifunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa umeme vijijini (Rea) Mhandisi Advera Mwijage,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki baada ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kufunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.
..................................................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Medard Kalemani,amesema kuwa, Serikali imeridhishwa na utendaji kazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wizara ya Nishati imekuwa ikijivunia utendaji kazi wao.
Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha kutathimini utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini kilichowashirikisha REA na TANESCO.
Dkt. Kalema amewataka REA kulinda hadhi yao kwa kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ambayo hayajafikishiwa huduma ya nishati ya umeme.
"Ndugu zangu mafanikio ya nchi hii yanategemea REA na TANESCO, vigezo vilivyofanya tuingie kwenye uchumi wa kati umeme umechangia kwa kiasi kikubwa sana" amesema Dkt. Kalemani.
Dkt.Kalemani amesema kuwa Serikali imeweka malengo na mipango yake kuhakikisha wananchi kila Kijiji wanapata nishati bora ya umeme hivyo muhakikishe vijiji vyote vinapata nishati ya umeme.
''Maeneo ambayo REA imekuwa na mafanikio ni kufikisha umeme katika vijiji 10,300 sawa na asilimia 87, kati ya vijiji 12,268 hapa nchini na lengo letu ni kuhakikisha vijiji vyote vinapata Nishati ya umeme''amesema Dkt.Kalemani
Naye , Naibu Waziri wa Nishati Wakili, Stephen Byabato,aliwapongeza REA kwa kufanya kazi nzuri ya usambazaji umeme nchini na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA), Mhandisi Advera Mwijage, amesema kuwa watahakikisha maagizo yote yaliyotolewa na Waziri wanayafanyia kazi ili wananchi wote wanufaike na nishati hiyo ya umeme.
Post A Comment: