Teddy Kilanga
Dk.Edward Hosea ameinuka kidedea katika uchaguzi wa nafasi ya urais wa chama cha mawakili wa kujitegemea Tanganyika (TLS)kwa kura 297 dhidi ya wagombea wenzie.
Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi,TLS,Charles Rwechungura amesema jumla ya wapiga kura ni 5286 na waliopiga kura ni 802 huku Flavian Charles akipata kura 223,Shehzad Walli kapata 192,Albert Msando 69 k na Flansis Stolla 17.
Kwa upande wake Dk.Hosea ambaye ameshinda kwenye kinyang'anyiro hicho alisema uchaguzi kwa mara ya kwanza umefika mbali na umekuwa wa haki na huru kwani umeonyesha ni kwa namna gani tasnia ya sheria ni muhimu sana katika maisha ya watanzania kwani wamekuwa wakifuatilia uchaguzi kutokana na kamati ya TLS pamoja na uongozi wake wote.
"Kwa kweli uchaguzi huu umekuwa wa kuigwa katika nyanja mbalimbali na mtazamo wangu kuanzia sasa tunaipeleka wapi TLS ikiwa kazi kubwa ya chama hicho ni kusimamia utawala wa sheria,mahakama zilizo huru huo ndio mtazamo wetu na mwelekeo wetu kuanzia sasa kwa kushirikiana na mamlaka zote pamoja na serikali,"alisema Dk.Hosea.
Alisema uhuru wa utawala wa sheria unamaana ambayo unaweza kugawa katika makundi manne ikiwa na maana kila mtu yuko huru katika macho ya sheria na isibague ikiwa ndio msingi wake ikiwa wao kama TLS kazi yao kubwa ni kutetea maslahi ya wananchi.
Naye Mshiriki wa uchaguzi huo ambaye ni mshindi wa pili na mwanamke pekee,Flavian Charles alisema ni jambo la kumshukuru Mungu ikiwa uchaguzi umeisha kazi iliyobaki ni kukitumikia chama chao cha TLS na uchaguzi ulikuwa mzuri na Amani usio na fujo lakini changamoto iliyojitokeza ni wanachama wengi kutoshiriki kupiga kura.
"Watu wengi walikuwa wakiongelea mitandaoni lakini cha kusikitisha jumla ya walioshiriki kupiga kura imekuwa idadi ndogo kulinganisha na idadi ya wanachama waliopo kwenye chama,"alisema.
Post A Comment: