Na Mwandishi Wetu, Singida
SHIRIKA la Umeme Kanda ya Kati (Tanesco) limetoa mafunzo ya siku tatu kwa Wahandisi (Engineer Forum) kutoka Mikoa ya Singida Dodoma na Morogoro.
Mafunzo hayo yanayofanyika mkoani hapa, yamelenga kuongeza ufanisi kwenye ufanyaji kazi za kila siku.
Akifungua mafuzo hayo Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Reymond Seya, alisema wahandisi ni watu muhimu sana katika ustawi wa uchumi wa Taifa.
"Sisi kama shirika la umeme hapa nchini lazima tuhakikishe umeme haukatiki katiki hovyo ili uchumi wa nchi yetu usonga mbele, nendeni mkafanye kazi kwa bidii." alisema Seya.
Akiendesha mafunzo hayo Meneja Mwandamizi wa Usambazaji wa shirika hilo, Athanasius Nangali alisema wapo hapo kwa ajili ya kupitia na kutazama majukumu yao kwenye utendaji wa kazi na kwamba baada ya mafunzo hayo watakwenda kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wateja wanapata umeme wa uhakika.
Post A Comment: