Teddy Kilanga
ARUSHA
SERIKALI imekitaka Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS )kuachakujihusisha na masuala ya kisiasa na uanaharakati badala yake kijikite zaidi kusaidia jamii katika nyanja za kisheria.
Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa TLS uliofanyika jijini Arusha,Naibu katibu Mkuu wa wizara ya Sheria na Katiba,Amon Mpanju,alisema
pamoja na Mambo mengine Mkutano huo utamchangua irais mpya kuchukua nafasi ya aliyemaliza muda wake huku akikitaka chama hicho kuendeleza misingi ya sheria.
Mpanju ambaye kitaaluma ni wakili,alisema kuwa kumekuwepo na Baadhi ya
Viongozi wanaochaguliwa na TLS kuendesha harakati za kisiasa na
kusahau majukumu yao Jambo hiloolisifanyike na chama hicho kijikite kutetea haki za wananchi.
Amewataka wanachama wa TLS wanaofikia 10,000 hapa nchini kuzingatia
maadili ya taaluma yao ,kuwa na mienendo mizuri Katika kufuata utawala
wa kisheria.
"Kuna mawakili wamekuwa na tabia ya kuchukua fedha za wateja wao na
kushindwa kuwawakilisha vizuri na wengine kutelekeza mashauri
yao,Jambo Hilo si jema Sana na wanapaswa kubadilika na kuzingatia
miiko ya kazi yao"alisema.
Katika hatua nyingine Mpanju ameonya mawakili wa serikali wapatao 1703
ambao Baadhi yao wanajihusisha na uwakili wa kujitegemea nje na
utaratibu, kuacha Mara moja na kuwataka wenye tabia hiyo kuchagua moja
Kati ya uwakili wa serikali ama kujitegemea.
Ameitaka TLS kujikita zaidi kwenye misingi ya kuendeleza tasinia ya
kisheria na Viongozi wanaochaguliwa wajitafakari na kuja na mbinu mpya
ya kuwatetea wananchi.
Awali Rais wa TLS anayemaliza muda wake, Dkt Rugemereza
Nshalla,amesema kuwa TLS imekuwa na Changamoto mbalimbali hali
iliyofanya kushindwa kufikia malengo yake Katika kipindi cha miaka
miwili.
Alizitaja Baadhi ya Changamoto hizo kuwa ni pamoja na mabadiliko ya
kisheria hapa nchini,Ugonjwa wa Corona ,Baadhi ya wanachama
kubambikiwa kesi zikiwemo za utakatishaji fedha,wanachama kutishwa na
wengine kufutiwa leseni ,kuhuisha leseni na kutakiwa kujisajili Kodi
ya ongezeko la thamani (VAT).
Hata hivyo dkt Nshalla alisisitiza kuwa TLS itaendelea kupigania na
kutetea haki za wananchi pamoja na wanachama wake ikiwemo wanachama
waliofungiwa leseni zao.
Chama hicho Cha wanasheria Tanganyika kinatarajia kufanya uchaguzi
hapo kesho(leo) kumpata rais mpya baada ya Dkt Nshalla kumaliza muda
wake,ambapo wagombea watano watachuana vikali kuwania nafasi hiyo
ambao ni Albert Msando,Dkt Edward Hosea,Flaviana Charles,Fransis
Stolla na Shehzad Walli.
Post A Comment: