MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wwakati wa futari na kugawa msaada wa vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Kiislamu cha Maawal kilichopo Jijini Tanga wenye thamani ya Milioni 4 katika halfa iliyofanyika Shule ya Sekondari Jumuiya vilivyotolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt Elirehema Doriye akizungumza mara baada ya futari hiyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt Elirehema Doriye katikati akigawa msaada  wa vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Kiislamu cha Maawal kilichopo Jijini Tanga wenye thamani ya Milioni 4 katika halfa iliyofanyika Shule ya Sekondari Jumuiya vilivyotolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kushoto ni Shehe wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt Elirehema Doriye katikati akigawa msaada  wa vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Kiislamu cha Maawal kilichopo Jijini Tanga wenye thamani ya Milioni 4 katika halfa iliyofanyika Shule ya Sekondari Jumuiya vilivyotolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kushoto ni Shehe wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt Elirehema Doriye katikati akipata futari sambamba na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari kushoto na Shehe wa Mkoa wa tanga Juma Luwuchu kulia iliyaoandaliwa na Shirika hilo na kufanyika shule ya Sekondari Jumuiya Jijini Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto aliyevaa suti nyeusi akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda wakipata futari ya pamoja iliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC)



MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu na kumuunga mkono ili anayotaka kufanya yawe makubwa zaidi kuliko kupindi cha miaka mitano iliyopita.

Aliyasema hayo wakati wa futari na kugawa msaada wa vyakula kwa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Kiislamu cha Maawal kilichopo Jijini Tanga wenye thamani ya Milioni 4 katika halfa iliyofanyika Shule ya Sekondari Jumuiya vilivyotolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Mkuu huyo wa Mkoa alisema serikali ni ya watu wasikivu wana kiongozi hodari ambaye ni msikivu mwenye huruma lakini ambaye hataki mambo ya mchezo na ambayo yanaweza kuwapoteza wananchi Maendeleo.

“Tunapoomba dua kwa ajili ya Rais wetu Samia Suluhu kwenye utendaji wake wa kazi nasi tujielekeze zaidi kwenye utendaji na uwajibikaji kwa kutimiza majukumu yetu maana ya kazi iendelee na alipojielekeza kwenye kazi iendelee maana yake juhudi kwenye ufanisi zinahitajika kuongezeka zaidi”Alisema

“ Lakini tuendelee kumuombea mwenyezi Mungu kwanza roho ya Marehemu Hayati John Magufuli mwenyezi Mungu aipokee na aihifadhi mahali pema peponi pia tumuombee Rais na kumuunga mkono ili aliyopanga kufanya yawe makubwa zaidi kuliko kipindi cha miaka mitano iliyopita “Alisema

“Pia tunapokuwa kwenye mfungo mtufuku tunamshukuru Rais Samia Sluhu yale maneno kuhusu bomba la mafuta sasa linakuja Jumatatu wiki hii walikuja wataalamu wa bomba la mafuta kueleza namna walivyofikia muda sio mrefu hatua ya kwanza itakuwa ni kulipa fiidia kwenye eneo lote bomba litakaopita”Alisema RC shigella.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema hatua ya pili ni kulipa fidia kwenye maeneo yatakayogusia kwenye ujenzi makambi na ujenzi wa Bandari Chongolea na ujenzi Matenki yakayatumika kuhifadhi mafuta hayo ambayo yatakuwa yakitokea Hoima nchini Uganda hadi Tanga.

Alisema miradi huo ni mikubwa na utengeneza ajira nyingi na fursa za kibiashara kwa wananchi hivyo wao kama serikali watahakikisha wanatenda haki kusimamia maslahi yao ambayo wanaweza kusimamia kwenye mkoa ili wananchi wao wawze kunufaika.

“Lakini kwa wale watakaopata biashara ya kusambaza mchanga,maji,chakula ,malori ya mafuta itakapokuwa inahitaji kuwekeza bima tusuitafue bima nyengine bali tuenda kwa Shirika la taiufa la Bima (NIC)”Alisema RC Shigella.

Awali akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt Elirehema Doriye alisema wameamua kuanza kuwafuturisha mkoa wa Tanga na wamezingatia wenye mahitaji muhimu ikiwemo yatima wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Alisema ndio maana wameamua kupelekea bidhaa hizo zenye thamani ya milioni 4 kwa watoto watakaotumia msaada huo utawasaidia.

“Nimshukuru sana Shehe wa Mkoa kwa kuendelea kujenga misingi ya ushirikiano na sisi watumishi wa serikali kazi inakuwa nyepesi kwenye misingi ya umoja unapokuwa na viongozi aina yako kazi ytu inakuwa nyepesi”Alisema

Mkurugenzi huyo alisema wamejumuika na waislamu katika mkoa wa Tanga kwa ajili ya kufuturisha watoto yatima na waislamu mwenye mwezi huu wa Ramadhani ikiwa ni sehemu mojawapo ya kurudisha kwa jamii .

“Kama sehemu ya jamii tunajumuika na jamii imekuwa ikiwatusapoti kwenye shughuli zetu na kuwasaidia wale ambao hawajapata bahati ya kuishi maisha wanayoiyategemea watoto yatima ambao hawana wazazi na wanahitaji misada ya kijamii”Alisema

Alisema msaada huo ni sehemu ya kuonyesha mshikamano wao kwa jamii ya waislamu ikiwemo kutekeleza baadhi ya maelekezo ya Rais Samia Suluhu ambapo kwenye kongamano la Viongozi wa dini alisema wanahitaji kushirikiana kwa pamoja kuwa na umoja na kujenga jamii bora.

Alisema pamoja na kufuturu nao lakini wametoa msaada kwa ajili ya watoto yatima Tanga ni mkoa wa Tanga na wataendelea kwenye mikoa mingine.

“Tunaheshimu ibada ambayo inaendelea ni pamoja na Sukari,Tende,Sabuni pamoja na mafuta na vitu vyote ambavyo vinaweza kuwasaidia kwenye mwezi wenye thamani ya milioni 4 na tutaendelea kutoa kwenye mikoa mingine”Alisema

Mwisho.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: