Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha  ACP-Justine Masejo akizungumza na waandishi wa habari

Na Woinde Shizza, -ARUSHA
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha mwezi januari hadi Machi 2021, lilifanya operesheni maalum ya kupambana na madawa ya kulevya katika mkoa wa Arusha ambapo limefanikiwa kukamata watuhumiwa 157waliokutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine, Bhangi na Mirungi.

Akionge na waandishi wa habari Kamanda w polisi mkoa wa Arusha ACP-Justine Masejo alisema kuwa kufuatia Operesheni hiyo walifanikiwa kukamata watuhumiwa 12 wote wa Kiume wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine kiasi cha gramu 536 na jumla ya kesi 11 zimefunguliwa na zipo katika hatua mbalimbali.

Alisema kwa upande wa madawa ya kulevya aina ya bhangi, kesi 81 zilifunguliwa ambapo jumla ya kilogramu 114 na gramu 624 zilipatikana pamoja na watuhumiwa 87 kukamatwa kati yao wanaume 76 na wanawake 11 huku akibainisha kuwa kesi hizo zipo katika hatua mbalimbali za kiupelelezi.

"Aidha katika operesheni hiyo tulifanikiwa kupata kilogramu 271 za Mirungi
ambapo jumla ya kesi 49 na watuhumiwa 58 walikamatwa kati yao wa
kiume 53 na wa kike ni 05 kesi hizo pia zipo katika hatua mbalimbali za
upelelezi."Alisema

Alibainisha kuwa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na operesheni kali dhidi ya wananchi wanaojihusisha na madawa ya kulevya pamoja na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya na kusema kuwa hawata sita kuwachukulia hatua kali za kisheria pindi tutakapo wakamata ambapo pia aliwaomba wananchi kushirikiana na nao ilikutokomeza kabisa matumizi na Biashara ya madawa ya kulevya

Alitoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo ya madawa ya kulevya ambapo aliwaomba wananchi wa mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa zinazohusiana na uhalifu na wahalifu ili mkoa uendele kuwa shwari asanteni.
Share To:

Post A Comment: