MBUNGE wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina ameshauri Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikaangalie kwa kina hoja
zote zilizoibuliwa kwenye taarifa ya CAG na kuhakikisha watuhumiwa wote
wamejumuishwa katika hatua ya kutoa adhabu kwa mujibu wa Sheria na
Kanuni zake ambazo ni Sheria za Fedha, Bajeti na Manunuzi.
Akizungumza
jijini Dodoma, Mpina ameshauri hoja zote zilizowasilishwa na CAG baada
ya uchambuzi wa Kamati ya PAC na LAAC ziandaliwe kwenye bangokitita
itakayoonesha hoja ilivyoletwa na uhalisia baada ya uchambuzi wa kamati
hizo ili ukweli ujulikane.
Mpina
amesema kwa mujibu wa taarifa ya CAG inasema usimamizi usioridhisha wa
Mfuko wa Tozo ya Maendeleo ya Utalii kuanzia mwaka 2019/20 na 2017/2018
bilioni 34.9
Imesema kiasi cha fedha sh. bilioni
5.4, sh. bilioni 2.8 na sh. milioni 100 zilihamishwa na Mkurugenzi wa
Utalii kwenda Bodi ya Utalii, Chuo cha Taifa cha Utalii na Makumbusho ya
Taifa bila idhini ya Afisa Masuuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mpina
amesema ripoti hiyo inasema kiasi cha sh. bilioni 6.9 zililipwa toka
kwenye Mfuko wa Tozo ya Maendeleo ya Utalii bila idhini ya Afisa Masuuli
wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kiasi
cha sh. bilioni 16.36 zililipwa bila ya kuwa na hati za malipo na
bilioni 11.156 zilikuwa na upungufu wa nyaraka na kwamba Malipo ya namna
hiyo ni kinyume na Kanuni ya 88 (1) za fedha za mwaka 2001 na Kanuni ya
9 (2) na 11 ya Kanuni za Tozo ya Maendeleo ya Utalii ya mwaka 2013.
Mpina
anasema hata hivyo CAG anapendekeza Mkurugenzi wa Utalii na Mhasibu
ndio wanahusika na usimamizi mbaya wa fedha za tozo la Mfuko wa
Maendeleo huku akimuondoa Katibu Mkuu wizara hiyo kwenye tuhuma hizo.
Mpina
amejiuliza fedha zilitokaje bila idhini ya Afisa Masuuli?, Miaka
miwili ya fedha mfululizo fedha zilitoka kwenye mfuko wa maendeleo ya
utalii bila afisa masuuli kujua? Kama ndivyo nafasi yake ya usimamizi
iko wapi.
Serikali
imeboresha mfumo wa ukusanyaji mapato na matumizi kwa kutumia njia ya
TEHAMA inawezekanaje fedha zote hizo zikatoka bila kuidhinishwa na
mamlaka husika?
“Shida
yangu hapa ni kwa nini wahusika wengine wanalindwa na kukikingiwa kifua
na taarifa ya CAG kinyume na Sheria ambazo amezinukuu yeye mwenyewe
ilihali watuhumiwa hao wanafahamika ili kukuza dhana ya uwajibikaji kwa
wote” anauliza Mpina
Hivyo
Mhe. Mpina ameshauri Kamati ya PAC ikaangalie kwa kina hoja hiyo na
kuhakikisha kuwa watuhumiwa wote wamejumuishwa katika hatua ya kutoa
adhabu.
Pia Hoja zote
zilizowasilishwa na CAG baada ya uchambuzi wa Kamati ya PAC na LAAC
ziandaliwe kwenye matrix itakayoonesha hoja ilivyoletwa na uhalisia
baada ya uchambuzi.
Pia
Mpina ameibua hoja nyingine inayohusiana na Maliasili na Utalii ni
pamoja na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA), zilifadhili Tamasha la upandaji Mlima Kilimanjaro
bila kuidhinishwa katika bajeti kiasi cha sh. Milioni 171.9.
Pia
TANAPA ililipa Kampuni ya Asante Tours and Safari’s sh. Milioni 57.4
kwa ajili ya gharama za malazi kwa wapandaji mlima ambapo ilibainika
kuwa kazi ilipatikana bila ushindani na hapakuwepo na mkataba
Ofisi
ya Waziri wa Maliasili na Utalii iligharamiwa na Mamlaka ya Hifadhi
Ngorongoro (NCAA) na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kiasi cha sh.
Milioni 148.2 bila fedha hizo kuwepo kwenye bajeti.
Mapendekezo
ya CAG hatua zichukuliwe kwa Waziri na Katibu wa Waziri huku akiwaacha
Maafisa Masuuli wote ambao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii na Watendaji Wakuu (CEO’s) wa TANAPA, NCAA na TFS.
Mpina
amejiuliza kwanini Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na
Watendaji Wakuu wa Mashirika ya TANAPA, NCAA na TFS wamekingiwa kifua na
ripoti ya CAG.
Pia
anayetangaza Zabuni na kuingia mikataba sio Waziri bali ni maafisa
masuuli kwanini adhabu ielekezwe kwa Waziri pekee. Fedha huidhinishwa
kutumika na maafisa masuuli na ndio wasimamizi wakuu wa bajeti kwanini
makosa yaelekezwe kwa Waziri peke yake.
Hivyo
ameshauri Kamati ya PAC ikaangalie kwa kina hoja hii na kuhakikisha
kuwa watuhumiwa wote wamejumuishwa katika hatua ya kutoa adhabu kwa
mujibu wa Sheria na Kanuni zake ambazo ni Sheria za Fedha, Bajeti na
Manunuzi.
Pia Hoja zote zilizowasilishwa na CAG
baada ya uchambuzi wa Kamati ya PAC na LAAC ziandaliwe kwenye
bangokitita itakayoonesha hoja ilivyoletwa na uhalisia baada ya
uchambuzi.
Post A Comment: