MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema Jimbo la Kisesa linachangamoto nyingi sana ikiwemo uvamizi wa tembo ambao wamekuwa wa muda mrefu bila kupata suluhisho kutoka serikalini

Amesema wananchi wanavamiwa na tembo mazao yao yanaliwa yakiwa shambani na hata yakiwa nyumbani chakula kinaliwa mashamba yote yanakanyagwa watu wamepoteza maisha wengine wamepata ukilema wa kudumu.

Mhe. Spika tumelalamika sana na tumeomba sana serikalini kulitatua hili tatizo lakini leo miaka mitatu sasa wananchi hao bado wanaendelea kwenye dhiki kubwa sana ya uvamizi wa tembo lakini uvamizi huu uko kwenye maeneo mengine pia

Mhe. Waziri Mkuu kwa sababu ni muda mrefu sana na tumekuwa tukipeleka malalamiko haya serikalini na hayajatatuliwa mpaka sasa hivi ambapo imepeleka umasikini mkubwa kwa wananchi tunaomba tatizo hili lifike mwisho.

Mhe. Spika tunajua Serikali hii tuliyonayo ya awamu ya tano na hii ya sita imetatua mambo mengi yaliyokuwa yameshindikana lakini imeweza kuyatatua mambo makubwa imeweza kuyatatua haiwezi kushindwa kuwazuia tembo.

Mhe. Spika tumeweza kumaliza mambo ya rushwa na ufisadi, tumeweza kumaliza madawa ya kulevya tumeweza kumaliza ujambazi na ujangili, tumeweza kumaliza uvuvi haramu tuje tushindwe na tembo”?

Mhe. Spika hapa kuna mtu mmoja hajawajibika sawasawa tunataka safari hii wananchi waishi kwa amani katika maeneo yao na tatizo hili la Tembo Mhe. Waziri Mkuu agiza likomeshwe mara moja.

Mhe. Spika tunalo tatizo pia kubwa sana la wafugaji ambao walikuwa wanafuga wakakamatwa na wahifadhi kwamba wanachungia ndani ya hifadhi na baada ya hapo wakaenda kushinda kesi mahakamani wakakatiwa rufaa wakaenda kushinda kesi mahakamani zaidi ya wafugaji 30 wenye ng’ombe wasiopungua 5,000 ng’ombe wao mpaka sasa hivi wanashikiliwa na Serikali licha ya kushinda kesi mahakamani.

Na wamefuatilia serikalini kurudishiwa mifugo yao kwa sababu wameshapewa haki hiyo na Mahakama warudishiwe mifugo yao lakini mpaka sasa hivi tunavyozungumza Mhe Spika ng’ombe hao hawajarudishwa na sababu za kutorudishwa hazijulikani mtu ameshinda kesi mahakamani kwanini uendelee kuzuia mifugo yake?.

Mhe. Spika kwa Jimbo la Kisesa peke yake ni zaidi ya ng’ombe 1,000 wanashikiliwa licha ya wananchi hao kushinda kesi mahakamani wananchi akina Malimi Sendama na wenzake, Ndaturu Malolo, Kwandu Malaba, Masunga Mhamali, Subi Maduhu na wengine Mhe. Waziri Mkuu tunataka kuambiwa huko Serikalini aliyekataa ng’ombe hizi zisitolewe ni nani kama mahakama imesha grant haki hao wafugaji aliyekataa huko serikalini ni nani?.

Mhe. Spika namuomba sana Mh. Waziri Mkuu aliingilie kati hili suala tukatende haki kwa hao wananchi wanyonge ambao mifugo yao imeshikiliwa na Serikali licha ya wao kushinda kesi mahakamani na tukitoka kwenye hili bunge niende na hizo ngombe za wananchi hawa


Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: