Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo amekabidhi saruji tani 29 kwa Afisa Elimu Msingi na Afisa Elimu Sekondari ili kusaidia ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari za Jiji la Dodoma.
Mbunge Mavunde amekabidhi saruji hizo zenye thamani ya Tsh 10,000,000 na kuwataka Walimu wakuu na viongozi wa kata husika kusimamia matumizi yake ili kufikia lengo lililokusudiwa.
“Mchango wangu huu ni kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu na hasa katika ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo sambamba na kuunga mkono jitihada za wananchi za ujenzi wa shule mpya za msingi na sekondari,hivyo lazima ninyi viongozi msimamie matumizi sahihi ya vifaa hivi.
Nitaendelea kuchangia kwenye sekta hii ya Elimu ili kuwafanya wanafunzi wa Dodoma Jiji wasome katika mazingira ambayo ni rafiki,lakini pia tunaishukuru serikali kupitia TEA kwa kutupatia Tsh Bilioni 1.9 za ujenzi wa madarasa na majengo ya utawala kwa shule 5 za msingi”Alisema Mavunde
Wakishukuru kwa niaba ya Wananchi,Madiwani Assedi Ndajilo-Hombolo Bwawani na Charles Ngh’ambMbalawala wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna anavyochangia maendeleo ya sekta ya Elimu katika kusaidia kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma na wametumia fursa hiyo kuahidi kusimamia vyema matumizi ya vifaa hivyo kwa malengo yakiyokusudiwa.
Akizumngumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji,Afisa Elimu Msingi *Ndg. Joseph Mabeyo* amemshukuru Mbunge Mavunde kwa mchango wake mkubwa kwenye sekta ya Elimu na kwa namna ambavyo amekuwa akishirikiana na Idara za Elimu Msingi na Sekondari Jiji kutatua changamoto mbalimbali.
Post A Comment: