Mbunge wa Viti maalum kupitia kundi la vijana Mhe. Asia Halamga akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita katika shule ya Dodoma Sekondari mapema jana.
Mbunge wa Viti maalum kupitia kundi la Vijana kutokea Mkoa wa Manyara Mhe: Asia Halamga akitoa hotuba yake alipokuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya kidato cha Sita katika shule ya Dodoma Sekondari hapo jana.Katika hotuba yake Mhe. Asia Halamga aliwahimiza vijana kutambua kwamba hivi sasa soko la ajira lina ushindani mwingi sana na hivyo yawapasa vijana kuthamini elimu na pia kupata ujuzi mwingine kama vile lugha za kigeni na kompyuta ili kuwa na sifa za kuajirika vizuri na pia kuweza kushindana vizuri katika sekta binafsi.
Post A Comment: