Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema suala la uadilifu na uzalendo enzi za Hayati Mwalimu Nyerere lilipewa kipaumbele sana na hivyo ilisaidia kujenga Taifa imara


Akizungumza  wakati wa  Kongamano Maalumu la Maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwalimu Julius K Nyerere amewataka watanzania kuyaishi maisha ya Baba wa Taifa kama ambavyo Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu kinafanya Kwa kutoa mafunzo ya uongozi na Maadili.


Prof. Ndalichako Pia amekitaka Chuo Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kifanye ufuatiliaji wa wanaohitimu mafunzo ya uongozi na Maadili katika Jamii kuona Je ni kweli wanafunzi wanaomaliza katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wanakuwa mabalozi wazuri.



Kupitia Kongamano hilo pia amezitaka Taasisi za Elimu  zifanye tathmini ya mitaala kama inafaa na kuendana na hali ya sasa, na kama ipo haja ya kuboresha basi maboresho ya yafanyike.


Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu nyerere Stephen Wasira amemzungumiza baba wa Taifa kuwa alikuwa ni mzalendo, muadilifu ambaye aliweka mbele maslahi ya Taifa la Tanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Prof. Shadrack Mwakalila amesema dira ya Chuo ni kuwa kitovu Cha utoaji mafunzo bora, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya uongozi na maadili pamoja na kufanya tafiti zenye lengo la kutatua changamoto katika Jamii.


Mafanikio ni mengi ikiwa ni pamoja na kuongeza udahili katika kampasi zote, Chuo kimeongeza idadi ya wahitimu, Chuo kimeongeza idadi ya watumishi, Chuo kimeongeza idadi ya programu za kitaaluma kutoka programu Tatu hadi kufikia kumi.


Mada Kuu ya Kumbukizi ni Kongamano Maalumu la Maadhimisho ya Kumbukizi ya baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius K Nyerere.


Imetolewa na:


Kitengo Cha habari na Mahusiano

13.04.2021

Share To:

msumbanews

Post A Comment: