Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi (katikati) akiwa na Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Yodas Mwanakatwe (wa pili kulia) na wajumbe wengine baada ya kufanyika kikao cha wasilisho cha pendekezo la mradi wa kilimo cha alizeti mkoani hapa kilichofanyika hivi karibuni. Kushoto ni Afisa Maendeleo Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani. Kulia ni Afisa Biashara wa benki hiyo, Willy Lyaumi na Afisa Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Wilaya ya Iramba, Marietha Kasongo
Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya TADB, Yodas Mwanakatwe, akisaini kwenye kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika kikao hicho.Kulia Afisa Biashara wa benki hiyo, Willy Lyaumi.
Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya TADB, Yodas Mwanakatwe, akizungumza na wajumbe wa kikao hicho.
Kikao kikiendelea. Kulia ni ni Afisa Maendeleo Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani.
Na Dotto Mwaibale, Singida
KAIMU Afisa Maendeleo Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani amewataka Vijana wa Mkoa wa Singida kuchangamkia fursa ya mkopo wa kilimo cha zao la alizeti unatolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
Ndahani aliyasema hayo baada ya kikao cha wasilisho cha pendekezo la mradi wa kilimo cha alizeti mkoani Singida kilichofanyika hivi karibuni mkoani hapa.
" TADB imetenga jumla ya Sh.millioni 767 kwa ajili ya kuvikopesha vikundi vya vijana ndani ya Mkoa wa Singida kwa kilimo kitakachofanywa kwa mtindo wa pamoja (Block farming)." alisema Ndahani.
Ndahani alisema maeneo yamekwishwa tengwa kwa ajili ya kilimo hicho hivyo ni vijana wenyewe wanatakiwa kujiunga kwenye kikundi na halmshauri ili kupewa utaratibu wa kupata mkopo huo.
Ndahani amewahakikishia vijana hao kuwa soko la alizeti ni kubwa ndani na nje ya mkoa wa Singida na kuwa nchi yetu inakabiliwa na upungufu wa mafuta ya kula ambapo 360,000 ujazo wa tani huagizwa kutoka nje ya nchi na kuwa uhakika wa soko upo ni wao vijana kuamua kujishughulisha na kilimo hicho.
Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya TADB, Yodas Mwanakatwe amewadhibitishia vijana kuwa wako tayari kushirikiana kuendeleza sekta ya kilimo na mifugo kwa kuwapatia mikopo ,ili lengo la Serikali na adhima ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutatua tatizo la ukosefu wa ajira liweze kutatuliwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhandisi Godfrey Sanga alisema mpaka sasa Halmshauri hiyoy imeshatenga eneo la ekari 3000 Kwa ajili ya kilimo cha alizeti kwa vijana ambao watapewa mkopo wa kilimo kutoka TADB.
Post A Comment: