Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ameitaka Kamati ya Ujenzi inayojenga Mradi wa Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Polisi mkoa wa Singida, kukamilisha mradi huo kwa muda uliokusudiwa ili liweze kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
IGP Sirro amesema hayo akiwa Mkoani Singida ambapo alikagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Polisi mkoani humo, mradi ambao unatekelezwa kupitia mfumo wa Nguvu kazi yaani Force Account na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa saba mwaka huu. IGP Sirro amekagua Mradi huo wakati akiwa safarini kuelekea mkoani Dodoma, akitokea mkoani Mara alilokua
Post A Comment: