Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilayani Arumeru yaendeea kungara kwenye Taarifa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa kupata Hati Safi katika ukaguzi wa hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya MERU kwa mwaka unaoishia tarehe 30 Juni, 2020.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri hiyo, Ndg. Emmanuel Mkongo  amesema siri ya kupata hati safi ni  matumizi ya fedha yanayozingatia Sheria,  Kanuni, Taratibu na Miongozo  ya Fedha za Umma pamoja na Watumishi kuzingatia weledi, uadilifu na maadili ya Utumishi wa Umma.


Mkongo amesema kuwa, Halmashauri inamkakati wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii  kuhakikisha inaendelea kupata hati safi.


Mkongo amewapongeza  kwa Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watumishi wote wa Halmashauri hiyo kwa kufanya kazi kwa  juhudi, ubunifu, maarifa hali iliyowezesha kupatikana kwa Hati Safi mara tatu Mfululizo. Amewataka waendele kuchapa kazi kwa kuzingatia weledi, uwajibikaji na uadilifu kwa kuweka mbele uzalendo na maslahi mapana ya Umma na Taifa.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: