Na,Jusline Marco;Arusha
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima amezindua mpango mkakati wa kudhibiti Malaria Kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini
Arusha, Kilimanjaro na Manyara ambapo pia amewataka wananchi kuhakikisha wanaweka mazingira yao safi na salama wakati wote.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Malaria Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Arusha Dkt. Gwajima amesema njia iliyobora ya kupambana na ugonjwa wa Malaria ni kila mmoja kuhakikisha anachukua hatua za kupambana na ugonjwa huo ikiwemo kutumia vyandarua vyenye dawa pamoja na kunyunyuzia viwatilifu koko katika kuta za Nyumba.
Aidha alisema kiwango cha Malaria nchini kimeshuka kwa 50% kutoka asilimua 14.5 mwaka 2015 na asilimia 7.5 mwaka 2017 na kufanya kiwango cha maambukizi kwa Tanzania bara kuwa asilimia 24.4, huku katika Mikoa ya Kigoma kukiwa na asilimua 24, Geita asilimia 17, Kagera na Mtwara kukiwa na asilimia 15 ambapo alitaja Mikoa ambayo ina kiwango cha chini ya asilimia 1 ya maambukizi ya Malaria kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Iringa na Njombe.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Hassan Kimanta katika maadhimusho hayo alisema kuwa hadi kufikia mwaka 2020 Mkoa wa Arusha umeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa chini ya asilkmia 1 huku idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Malaria vikiwa vimepungua kwa asilimia 80 kutoka vifo 20 kwa mwaka 2015 hadi vifo 4 mwaka 2020.
Kimanta aliongeza kuwa idadi ya wagonjwa imepungua kutoka wagonjwa 15150 mwaka 2015 hadi kufikia wagonjwa 9314 mwaka 2020 sawa na punguzo la asilimia 35 ambapo alisisitiza kuwa mpango mkakati wa Mkoa wa Arusha ni kutokomeza ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030.
Awali maadhimisho hayo yalitanguliwa na ziara fupi ya kutembelea Zahanati ya Momela iliyopo jatika kata ya Ngarenanyuki Wilayani Arumeru ambapo Dkt.Gwajima alipata fursa ya kuzunguza na wanakijiji wa kata hiyo pamoja na muwekezaji (Afrika Amini Alama) ambaye alijenga na kutoa Huduma za afya Katika Zahanati hiyo baada ya kupata malalamiko toka kwa wakazi wa eneo hilo wakidai muwekezaji huyo amesimamisha baadhi za Huduma za afya na hivyo kuzorotesha huduma hizo baada ya kutokea kwa mgogoro baina yake na halmashauri hiyo.
Kutokana na hali hiyo Dkt.Gwajima aliweza kutoa elimu kwa wananchi juu ya mwongozo wa Ubia na ushirikiano wa Sekta ya Umma na Sekta binafsi(PPP) katika kutoa huduma za afya na ustawi wa Jamii Tanzania
Sambamba na hauo Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani huadhimishwa kila ifikapo Aprili 25 ambapo kwa mwaka huu 2021 kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika katika Mkoa wa Arusha na kuzinduliwa kwa mpango Mkakati wa kutokomeza Malaria nchini ifikapo 2025 kwa asilimia 3.
Post A Comment: