NA MWANDISHI WETU


MKUU wa ya Ilala Arch,Ng' wilabuzu Ludigija   anatarajia kuzindua Kampeni ya TABATA ya Kijani kwa kupanda miti Shule ya Msingi Tabata JICA wilayani Ilala. 


Akizungumza na Waandishi wa  habari Tabata Dar es salaam  Mwandaaji wa Kampeni hiyo Balozi wa Mazingira HERI SHAABAN ambaye ameshirikiana na Ofisi ya Serikali ya Mtaa TABATA Mtambani alisema katika tukio hilo watakuwepo Mgeni Mwalikwa  Meya wa Halmashauri ya Jijj Dar es salaam Omary Kumbilamoto.


 Balozi wa Mazingira HERI SHAABAN alisema uzinduzi huo utafanyika jumatatu saa mbili asubuhi shule ya jica .


"Kampeni ya uzinduzi WA TABATA ya Kijani imeandaliwa na ILALA yetu kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa Tabata Mtambani kwa dhumuni la kutunza Mazingira "alisema Heri



Heri alisema Kutunza mazingira ni jukumu letu sote kampeni hiyo ya TABATA ya kijani ni endelevu  dhumuni lake kuunga mkono juhudi za serikali katika suala zima la utunzaji mazingira. 


Alisema   vyanzo vya maji vinategemea miti hivyo kampeni hiyo inawataka WANANCHI kila wanapokata mti mmoja wapande miti mitano    kwani miti ina kazi nyingi ikiwemo Tiba Asili. 


Aliwaomba Wakazi wa TABATA kuunga mkono Kampeni ya uzinduzi wa TABATA ya kijani kupendezesha Shule zetu za Tabata  zilizopo wilayani Ilala ziwe na mazingira bora kwani mazingira bora  ya Shule yanaongeza Ufaulu kwa Wanafunzi pia ukuza taaluma.


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa TABATA Mtambani Brigita Nchimbi alisema  Maandalizi yote yamekamilika katika uzinduzi huo amewataka wakazi wa TABATA na Kata za jirani kujitokeza kwa wingi siku ya Jumatatu kuunga mkono Serikali katika suala zima la utunzaji wa Mazingira kwani una faida nyingi ikiwemo kuwapatia WANANCHI hewa safi. 


Mwisho

Share To:

msumbanews

Post A Comment: