NA HERI SHABAN(ILALA )


HALMASHAURI Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala   imeanza mchakato wake wa kuomba Wilaya mpya na Kugawa Majimbo ya Uchaguzi na Kata.


Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ubaya Chuma wakati wa kikao cha Halmashauri kuu kilichokuwa kinapokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani. 


"Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM Ilala wamelizia kugawa Majimbo ya uchaguzi pamoja na Kata kuanzia mitaa  na kuundwa kwa hamashauri mpya ndani ya Wilaya Ilala "alisema Chuma


Chuma alisema suala la Kugawa mipaka na Majimbo linaitaji busara na vikao vyenu zile Kata zenye shida WANANCHI wawashirishe  katika WDC .


"Ninaagiza zile kata zenye migogoro ya ardhi zipatiwe ufumbuzi wake haraka sisi wote ni wamoja na Wakuu wa Idara wanatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi hivyo msiwaogope naomba mshirikiane nao kwa pamoja "alisema


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Ilala Arch Ng'wilabuzu Ludigija aliwasilisha Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM 2020/2025 January  Machi 2021 alisema wilaya hiyo wamefaulisha kwa kiwango kikubwa ambapo wametenga shilingi Bilioni tatu kwa ajili ya madarasa .


Mkuu wa wilaya Ludigija alisema Masoko makubwa na Barabara zimekamilika Yombo na Kiwalani ambapo ni mkombozi kwa WANANCHI wa Ilala na maeneo ya kata za jirani  


Aidha sekta ya maji miradi yote imekamilika 

Kuhusu Barabara za TARURA wametumia sh, Bilioni 7.2 kwa ujenzi wa Barabara .


Kuhusu mradi wa Umeme wa REA Jimbo la UKONGA mradi wa Bilioni 25 mahitaji ya Msongola na Buyuni ni makubwa zimeongezeka bilioni 3.8.


Meya wa hamashauri ya Jiji la Dar es salaam  Omary Kumbilamoto amempongeza Mkurugenzi wa Jiji Mkuu WA wilaya Ilala pamoja na wakuu wa idara kwa ushirikiano wao


Meya Kumbilamoto aliwataka washirikiane pamoja katika kufanya kazi na kusimamia miradi ya Maendeleo ili kumsaidia Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA kukuza  uchumi wa viwanda.


Mwisho

Share To:

msumbanews

Post A Comment: