Msajili Msaidizi kutoka  Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),  Benedickson Wilson akitoa mada   kwa wafanyabiashara  wa Mkoa wa Singida.


Mafunzo yakiendelea. 

Maswali yakiulizwa kwenye mafunzo hayo.



Na Dotto Mwaibale,  Singida


WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) imetoa mafunzo ya siku mbili kwa wafanyabiashara mkoani  hapa kwa ajili ya kuwajengea uwezo.


Mafunzo hayo ya siku mbili kwa wafanyabiashara hao mkoani hapa yaliyoanza jana yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa RC Mission. 

Akizungumzia mafunzo hayo Msaidizi wa ofisi Mwandamizi Utawala kutoka Brela Saada Kilabula alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uelewa wafanyabiashara na kuwa yameanza hapa Singida na baadaye Dodoma na kuhitimishwa mkoani Morogoro.

" Kwa awamu hii ya kwanza tumeanzia hapa mkoani lakini hapo baadaye tunatarajia  kuyafanya mafunzo haya hadi ngazi za wilaya na lengo hasa wananchi wawe na uelewa wa kibiashara." alisema Kilabula. 

Alisema Brela iliona kuna haja ya kutoa mafunzo hayo kwa wananchi kutokana na baadhi ya watu wasiowaaminifu kuwatoza fedha nyingi wananchi wanapohitaji kusajili biashara zao hivyo kupitia mafunzo hayo yataondoa huo usumbufu na kutambulisha mfumo wa namna ya kujasili biashara kupitia simu za mkononi. 

“Hatujawahi kutoa mafunzo haya lakini tuliona kuna haja ya kuja huku chini kwa wananchi tuwape elimu kutokana na wengi kutozwa fedha nyingi wanaposajili biashara zao na baadhi ya watu wasiowaaminifu.” alisema Kilabula.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akifungua mafunzo hayo ameitaka BRELA kutoa semina ya biashara kwa viongozi wa Serikali na dini ili kuwa na uelewa kutokana na wao kukutana na watu wengi jambo litakalosaidia wananchi kuwa na uelewa wanapofanya biashara zao.  

Alisema wananchi wanachokihitaji sio kuifahamu Brela bali kupata matokeo chanya kwenye biashara zao kupitia Brela hivyo kupitia mafunzo hayo anategemea kuona mabadiliko makubwa.


Share To:

Post A Comment: