Waziri
wa Maji Jumaa Aweso (mwenye shati la bluu katikati) akiwa kwenye ziara
ya kukagua mradi wa Maji Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wa tatu kushoto
ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
|
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametembelea ujenzi wa mradi wa maji Mwakitolyo uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga huku akitoa siku 10 mradi huo uwe umekamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.
Amesema kati ya miradi ya maji 177 ambayo ni kero hapa nchini, mmoja wapo ni mradi huo wa Mwakitolyo hivyo kuagiza hadi ifikapo Mei 5 mwaka huu ndani ya siku 10 zijazo, uwe tayari umeshakamilika.
"Mradi huu wa maji Mwakitolyo nina historia nao, ni kati ya miradi ya maji kichefuchefu hapa chini, hivyo naagiza hadi ifikapo Mei 5 uwe tayari umeshakamilika”
“Nakumbuka nilikuja hapa miaka ya nyuma mradi hiu ulikuwa ni changamoto nikaupa jina kichefu chefu kwa sababu haiwezekani zitokea fedha Bilioni 1.4 lakini mwananchi hana maji “Alisema
Waziri Aweso alisema mradi huo ni miongoni mwa 177 ambayo waliianisha ambayo ilikuwa inachafua wizara na maelekezo yalikuwa ni kuhakikisha miradi kichefu chefu yote inakwamuliwa na kati ya miradi 177 miradi 85 wameikamilisha ikiwemo huo wa Mwakitolyo .
Alisema hivi sasa hapo hakuna kisingizio kwa sababu fedha zimekwisha kutolea milioni 400 na mabomba yameshajengwa hivyo ndani ya Mei 10 mwaka huu wananchi wanakwenda kupata huduma ya maji.
“Hapa visingizio hakuna tena tutakwenda kugombana kwa hali ninavyoiona mambo ni mzuri kubwa ninaloliona pamoja na wananchi wa mwakitolyo kupata maji lakini na mwakitolyo maeneo ya jirani inakuwa kwa kasi sana kwa hiyo tutafute eneo la mlima tutengeneze tenki la lita laki tano”Alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) Mhandisi Joshua Mgeyekwa, ambao ndiyo watekelezaji wa mradi kwa kushirikiana na (RUWASA),alimhakikishia Waziri Aweso kuwa utakamilika ndani ya siku hizo 10.
Post A Comment: