Meneja Mkuu wa Kampuni ya Shanta Singida Mhandisi Philbert Rweyemam (kushoto) na kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba wakiwa kwenye kikao kati ya Kampuni hiyo na Waziri wa Madini kilichofanyika katika Ukumbi wa Utawala Chumba namba 31 uliopo Bungeni jijini Dodoma Machi 30, 2021.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake walioshiriki kikao kati ya Waziri wa Madini na Uongozi wa Shanta kilichfanyika katika Ukumbi wa Utawala Chumba namba 31 uliopo Bungeni jijini Dodoma Machi 30, 2021.
Na Tito Mselem Dodoma,
Waziri
wa Madini Doto Biteko ameuagiza uongozi wa Wizara ya Madini kukutana na
viongozi pamoja na wanasheria wa Kampuni ya Shanta ili kuwajengea
uelewa juu ya Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika Sekta ya
Madini.
Hayo, ameyasema
leo Machi 30, 2021 alipokutana na Kampuni ya Shanta kujadili suala la
gawio la asilimia 16 linalotakiwa kutolewa kwa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Waziri
Biteko amesema, Kampuni ya Shanta ilete Wanasheria wake ili Wanasheria
wa Wizara watoe mafunzo na maelekezo ya Sheria, Kanuni na Taratibu
zilizopo katika Sekta ya Madini.
Aidha,
Waziri Biteko amesema, tumuenzi aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ndoto zake
za kufungua kwa wingi migodi ya uchimbaji wa madini ili Nchi iweze
kuwanufaisha watanzania.
Pia,
Waziri Biteko amewataka viongozi wa Kampuni ya Shanta kuhakikisha
wanaanza kazi ya uzalishaji haraka ili waweze kusaidia wananchi
wanaozunguka eneo hilo ikiwemo upatikanaji wa ajira kwa watanzania.
Vilevile,
Waziri Biteko ameutaka uongozi wa Kampuni ya Shanta kutoa gawio la
Serikali la asilimia 16 kwa mujibu wa Sheria ya Madini inavyoelekeza.
Awali,
Waziri Biteko, alimpongeza aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango kwa kuteuliwa na kupigiwa kura na wabunge kuwa Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Post A Comment: