Jane Edward,MsumbaNews, Arusha
Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya habari,Dokta Faustine Ndugulile ameitaka makao makuu ya posta Afrika kuhakikisha,huduma wanazotoa zinakuwa za kidigitali zaidi.
Akizungumza katika hafla hiyo ya kukabithi hati hiyo kwa umoja huo,Dokta Ndugulile amesema kuwa, kitendo hicho cha kukabidhi hati hiyo kimeleta manufaa makubwa Sana kwani kukamilika kwa mradi huo kutaleta tija kubwa Sana kwa umoja huo sanjari na kutoa nafasi za ajira kwa watanzania
So
Amesema kuwa ,mradi huo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shs 33.6 bilioni , ambapo aliipongeza wizara ya ardhi kwa kufanya kazi nzuri ya kukabithi hati hiyo kwani kwa muda mrefu walikuwa hawana hati ya kiwanja hicho.
Aidha alilitaka shirika hilo kuwa kielelezo pekee cha maendeleo ambacho kitakuwa mfano bora wa kuigwa huku akiwataka kwenda na kasi mpya ,na kuhakikisha makao makuu ya posta yanafafana huduma wanazotoa katika kuhakikisha inaendeshwa kidigitali zaidi.
"Tunawaomba Sana wakandarasi mnaosimamia huu mradi mhakikishe unamalizika kwa wakati kama ilivyopangwa mwezi wa sita ,2022 hivyo mhakikishe mnafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mnamaliza mradi huu kwa wakati na hakikisheni mnaongeza spidi zaidi ."amesema Waziri.
Naye Mwenyekiti wa bodi kutoka TCRA,Dokta Jones Killimbe amesema kuwa,ujenzi wa jengo hilo ambao ndio utakuwa makao makuu ya posta Afrika na ofisi za Kanda ya kaskazini za PAPU ni ushindi mkubwa Sana kwao kwani unaongeza ajira kwa watanzania walio wengi pia.
Post A Comment: