WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akizungumza leo mjini wakati akifungua kikao kazi cha wadau wa maji Mkoa wa Tanga kilichofanyika wilayani Lushoto |
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa kikao hicho kulia ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa kikao hicho |
MENEJA wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Omari akizungumza wakati wa kikao hicho |
MKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza jambo wakati wa kikao hicho |
MKURUGENZI wa Bonde la Maji la Pangani Segule Segule akifuatilia kwa umakini kikao hicho
Wadau wa kikao hicho wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso
Wadau wa Kikao hicho wakifuatilia masuala mbalimbali
Waziri wa maji Jumaa Aweso amezitaja sababu zilizokuwa zikikwamisha miradi ya maji kuwa ni kutokana na kuwatumia wakandarasi wababaishaji na wasiokuwa na uwezo.
Waziri Aweso ametoa, sababu hiyo wakati akifungua kikao kazi cha wadau wa maji Mkoa wa Tanga kilichofanyika wilayani Lushoto.
Waziri
Aweso alisema wakandarasi wasiokuwa na uwezo walikuwa wakipewa zabuni
kwa kujuana na hivyo kusababisha kusababisha miradi ya maji kutokamilika
na hatua hazichukuliwi.
Alisema
wizara hiyo hivi sasa imeondokana na changamoto hiyo baada ya kuweka
mikakati ya kuhakikisha wakandarasi wa namna hiyo hawapati nafasi.
"Wataalamu
walikuwa wakijua wazi kuwa baadhi ya wakandarasi walikuwa hawana uwezo
lakini bado walikuwa wakiwatumia na kuwaacha wale wenye
uwezo,"alibainisha waziri Aweso.
Sababu
nyingine iliyokuwa ikikwamisha miradi hiyo ya maji ni michakato
isiyokuwa na ulazima ambayo ilikuwa ni kikwazo kikubwa cha ukamilishaji
wa miradi mbalimbali nchini.
Aliwaagiza,
watendaji kayika, wizara hiyo kuacha visingizio badala yake watekeleze
wajibu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ameipongeza wizara
hiyo ya maji kwa kujitahidi kufikisha maji katika maeneo yaliyokuwa na
changamoto kubwa ya maji katika Mkoa Tanga.
Naye
Meneja wa Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) Mkoa
wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo katika kutekeleza, bajeti ya mwaka wa
fedha 2021/22 Ruwasa Mkoa Tanga inategemea kutumia jumla ya shilingi
38,437,802,839.39 ingawa mahitaji halisi ni shilingi 41,872,700,424.04
ili kukamilisha ujenzi wa miradi inayoendelea.
Alisema miradi hiyo ni pamoja na ukarabati wa miradi chakavu, usanifu na ujenzi wa miradi mipya.
"Ruwasa
Tanga inajumuisha wilaya zake 7 na inategemea kutekeleza ujenzi miradi
ya mipya ya maji kukarabati ya zamani kupanua miradi inayoendelea na
kusanifu miradi mipya kwa kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2021/12.
Kikao hicho kilikuwa na lengo la kufanya tathimini pamoja na kuangalia hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwenye miradi ya maji.
Mwisho.
Post A Comment: