Bwana shamba mwezeshaji vikundi kutoka
asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo horticulture yaani mboga, matunda, mimea itokanayo na mizizi, pamoja na viungo (TAHA)Meshack Marko wa kushoto akimuelekeza mkulima wa zao la hoho Joyce Samweli jana namna ya kupalilia na kuweka mbolea Katika zao lake aliloliotesha Katika Kijiji Cha Oloigerumo kilichopo Katika kata ya ilkiding'a Wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Mkulima kutoka kikundi kinachosimamiwa na asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo horticulture yaani mboga, matunda, mimea itokanayo na mizizi, pamoja na viungo (TAHA)Joyce Samweli kutoka kijiji cha Oloigeru kilichopo kata ya olkiding'a wilayani Arumeru mkoani Arusha akionyesha moja wanmfugo wake alionuna kutokana na fedha alizozipata kwenye kilimo.
 Joyce Samweli akionyesha baadhi ya mbegu za viazi ambazo ameziandaa kwa ajili ya kuziotesha.



Na Woinde Shizza, Arusha
WANAWAKE wametakiwa kuacha kukukaa majumbani na kuwa tegemezi badala yake wachangamkie fursa mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo kilimo ili waweze kujikwamua kimaisha .

hayo yameelezwa jana na mkulima kutoka kikundi kinachosimamiwa na asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo horticulture yaani mboga, matunda, mimea itokanayo na mizizi, pamoja na viungo (TAHA)Joyce Samweli alipokuwa anaongea na waandishi wa habari shambaini kwake katika kijiji cha Oloigeru upno kilichopo kata ya olkiding'a wilayani Arumeru mkoani Arusha akielezea mafanikio aliyoyapata kama mwanamke kuelekea katika siku ya wanawake duniani .

Alisema kuwa kuelekea siku ya wanawake duniani ni vyema wanawake wote hapa nchini washiriki vyema Katika ujenzi wa taifa ,kwani wao Kama wanawake wananchango mkubwa sana Katika ujenzi wa taifa , wanawake wananchango mkubwa sana Katika maendeleo ya taifa na nivyema wamsaidie kwa nguvu zote rais wetu kwa kuwa na malengo yake ni yenye neema tele kwa nchi yetu.

Alisema kuwa ni vyema wanawake wakaacha kukaa nyumbani na kutegemea kuletewa na wanaume wao badala yake waamke waanze kufanya kazi mbalimbali zinazojitokeza ili waweze kujiiingizia kipato kitakacho muwezesha kusaidia familia .

"mimi kwa upande wangu nimewekeza katika kilimo na nashukuru sana Taha wameweza kunielimisha vyema nikaweza kuaachana na utegemezi , nikiwa kama mwanamke niliamka na nikaamua kuanza kulima kilimo cha kawaida lakini Taha walivyokuja na kutuelimisha zaidi nimeweza kujishughulisha na kulima kilimo cha kisasa ambacho kimenisaidia kwa kikasi kikubwa kwani kupitia ,kilimo hichi nimeweza kujenga nyumba yangu ambayo kwa sasa inawapangaji pia nimeweza kununua mifugo ambayo kupitia hivyo ninajipatia maziwa ambayo nayauza na pia mbolea ambayo nairudisha shambani kwa ajili ya kilimo ."Alibainisha Joyce

alisema kuwa nivyema wanawake wasikae kwa kutegemea kupokea bali wapambane kutafuta pesa na washirikiane na familia zao kwaajili ya kujenga uwezo kifamilia .

Aidha alifafanua kuwa awali alipoanza kulima alikuwa akipata gunia 30 za vitunguu katika shamba la nusu heka lakini mara baada ya kukutana na Taha ,na kuelimishwa kuhusiana na kilimo cha kisasa ameweza kulima katika heka hiyo hiyo moja na kupata magunia 60 hadi 70 ya vitunguu kitu ambacho kimemfanya aishukuru Taha maana ndio mkombozi wake .

Alitoa wito kwa serikali kuwaangalia wakulima wadogo haswa waliopo vijijini kuwawezesha kupata pembejeo za kilimo kwa urahisi na kwa bei nafuu ,pia kuwasaidia wakulima kupata maeneo makubwa zaidi kwa ajili ya kufanya kilimo cha kisasa ili waweze kujikwamua kimaisha pia kuihingizia serikali fedha ambazo zitasaida kuleta maendeleo .

Akiongelea kwa njia ya simu mkulima wa zao la papao kutoka mkoani Mwanza Epiphania Buhogwa alisema kuwa yeye kama mwanamke anajivunia kuwa mkulima na anaishukuru sana TAHA kwa kumuelimisha kulima kilimo cha kisasa kwani kimeweza kumsaidi kuondokana na utegemezi ambapo pia aliwataka wanawake wengine kutokata tamaa katika jambo lolote ambalo wanataka kufanya .

"hakuna kukata tamaa ukiwa kama mwanamke ukiamua kufanya kitu ni vyema ukafanya na usikubali kurudi nyum kabissa mimi ,awali nilikuwa nimekata tamaa laki nilivyokutana na Taha walinipa matumaini mapya wakanielimisha namna ya kulima kilimo cha kisasa na kwakweli kimenisaidia sana na navyoongea hapa nimeweza kulima kilimo cha mapapai ni katoka na sasa nalima kilimo cha pasheni hivyo niwatake wanawake wenzangu kuacha kubweteka na badala yake kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo hususa ni katika kilimo maana kilimo hakimtupi mtu "alibainisha Epiphania

alibainisha kuwa awali alipoanza kulima alikutana na matatizo mbali mbali ikiwemo upatikanaji wa masoko ,wakulima kushidwa kujua magonjwa yanayoshambulia mazoa lakini kwa sasa matatizo hayo yameisha mara baada ya wataalam wa kilimo kutoka Taha kuwatembelea kuwashauri pia kuwatafutia masoko.

alitoa wito kwa serikali kuwasaidia wakulima h wadogo ambao wapo makini mitaji ambayo itawasaidi kuendesha kilimo cha kisasa kwani kilimo cha kisasa kinagharama kubwa ambapo kwa mkulima wa kawaida hawezi kuzimudu bila kusaidiwa ,pia aliitaka serikali kuangalia namna ya kuwasaidia katika kilkimo cha umwagiliaji ili wakulima wasilime kilimo cha kutegemea mvua za msimu.

Naye Bwana shamba mwezeshaji vikundi kutoka asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo horticulture yaani mboga, matunda, mimea itokanayo na mizizi, pamoja na viung (TAHA)Meshack Marko alisema kuwa asasi yao inavikundi 33 vya wakulima wa mazao ya mboga ,matuna na mmea itokanayo na mizizi na vikundi hivyo vinazaidi ya wanachama 2700 kati ya wananchama hao wanawake ni wengi zaidi kwani kuna jumla ya wanawake 1570 na hii inaonyesha ni namna gani wanaweke wameaacha kukaa na kuwa tegemezi na wamejiingiza katika kilimo .

Alibainisha kuwa wao kama Taha wamekuwa wakitoa elimu ya ugani ambayo ni namna ya kuandaa shama ,umuhimu wa kutumia matuta,kuwaelimisha kuhusiana na mbegu sahihi ,kupanda kwa nafasi , utumiaji bora wa viuwatilifu ambapo pia alisema wanazingatia vigezo vya usalama wa chakula zaidi .

Aliwataka wanawake wengi wajitokeze kuwekeza katika kilimo kwani kilimo kinaondoa watu katika umaskini pia kilimo kinafaida iwapo mkulima atalima kilimo cha kisasa kwa kufuata ushauri wawataalam wa kilimo
Share To:

Post A Comment: