Teddy Kilanga


Arusha


Kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa jamuhuri ya muungano Wa Tanzania Dk.Magufuli kilichotokea mnamo machi 17 na kuzikwa machi 26,Diwani wa kata ya sekei,Gerald Sebastian amewaomba wananchi kuwa wazalendo pamoja na kushirikiana na uongozi kuanzia ngazi ya chini hadi juu ili kusaidia kuleta maendeleo katika jamii na nchi kwa ujumla.


Akizungumza na waandishi wa habari,jijini Arusha,Diwani Sebastian alisema Dkt.Magufuli alikuwa mwalimu katika maisha ya uongozi kwani alijikita katika kuleta maendeleo ikiwa hali ya uchumi imebadilika na miundombinu  mbalimbali imekamilika ikiwemo barabara pamoja na uelewa wa haki kwa wananchi.


Diwani Sebastian alisema kuwa Dkt.Magufuli aliweka heshima katika ofisi za serikali katika kuwahudumia wananchi ambapo hapo awali walikuwa wakinyanyasika katika kupata huduma hivyo wanamatumaini na Rais ,Samia Suluhu katika kukamilisha miradi aliyowaachia.



Hata hivyo Sebastian alisema ni vyema wananchi wakaendeleza ushirikiano na mshikamano pamoja na kuwa wazalendo na nchi yao wenye lengo moja la kufikia uchumi wa kwanza.


"Dkt.Magufuli amenifunza mengi sana ukiangalia jiji la Arusha limebadilika kuanzia hali ya kiuchumi kutokana na uongozi wake wa kujiamnini kwa kutekeleza miradi mbalimbali kwa kuanzia miundombinu ya barabara na hata kipato pamoja na uelewa wa haki zao wananchi,"alisema.


mmoja wa wakazi wa jiji la Arusha ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini ,Magembe mbesi alisema hayati Dkt.Magufuli alikuwa ni jembe kwani amesaidia madini kutokutoroshwa na ameweka nidhamu serikalini hivyo ni vyema Rais,Samia akafuata nyenzo zake ili kuendelea kumuenzi kwa kuchapa kazi.


"Tunaomba viongozi walioko katika nafasi za juu kuchunguza kwani Dkt.Magufuli alikuwa anafuatilia kuanzia ngazi za chini hadi juu hivyo ni vyema Rais.Samia Suluhu Hassan awe jasiri na asiishie kusikiliza maoni ya watu ili nidhamu maofisini iendelee ,"alisema.

Share To:

Post A Comment: