Katibu Mkuu wizara ya maji, Anthony Sanga Akizungumza wakati alipotembelea mradi wa maji kutoka Longido kwenda Namanga pembeni yake ni viongozi mbalimbali wa Wilaya hiyo wakimsikiliza wakati akitoa maelekezo 


SERIKALI imewataka wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchiniambapo miradi ya maji inatekelezwa kuhakikisha kuwa wanailinda miradihiyo na kuwafichua wale wote wanaohujumu miundombinu ya miradi hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya maji,mhandisi Antony Sanga aliyasema hayo alipokuwa akikagua utekelezaji wa mradi wa maji kutoka Longido hadi Namanga pamoja na kupokea mabomba ya kusafirisha maji hayo katika kijiji cha Kimokouwa wilayani hapa.

Alisema kuwa Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kuhakikisha kuwa inawaondolea adha kubwa wananchi ya upatikanaji wamaji safi na salama pamoja na kuwaepusha na usumbufu wa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo hivyo ni jukumu lao kuilinda na kuitunza miradi hiyo.

Mhandisi Sanga aliiagiza mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha ambao ndio watekelezaji wa mradi huo kuhakikisha kuwa mradi huo unatekelezwa kwa viwango na ubora wa hali ya juu na waukamilishe kabla ya muda waliowekewa kwani rasilimali zote wanazo.

“Mradi huu ambao ulipangwa ukamilike mwezi wa nane mwaka huu hakikisheni hadi mwezi wa sita unakuwa umeishakamilika ikiwa ni pamoja na kutoa kazi za kuchimba mitaro na nyinginezo kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ambayo mradi huu unapita”alisisitiza katibu mkuu huyo.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo kwa Katibu Mkuu,Mkurugenzi mtendaji wa AUWSA,Mhandisi Justine Rujomba,alisema kuwa mradi huo ambao hadi kukamilika utatumia shilingi bilioni 4.8  tawanufaisha wananchi wa vijiji vya Kimokouwa,Orendeki na Namanga.

Aliongeza kuwa mradi huo umetoa maji katika mto Simba uliopo Kilimanjaro hadi Longido umbali wa kilomera 100 na kwamba Kutoka Longido hadi Namanga ni kilometa 43 na kwamba mpaka sasa
wameishachimbia mabomba kilometa kumi na utekelezaji wa mradi unaendelea.

“Mheshimiwa katibu Mkuu tunapokea bomba za nchi nane zenye urefu wa kilometa moja na kwamba magari mengine yako njiani yakiendelea kuleta mabomba na tunakuhahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi na hadi mwezi wa sita utakuwa umekamilika

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Longido,Juma Mhina aliipongeza serikali kwa kuwapatia mradi huo wa maji kwani utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo ambao yao wamekuwa wakipata adha kubwa ya kutembea umbali mrefu
kufuata huduma hiyo.

“Baada ya mradi huu kukamilika utawanufaisha wananchi elfu kumi na mbili wa Wilayani hapa ambapo pia tutaoa matoleo ya maji kwa wananchi wenye adha ya maji katika maeneo ambayo mradi unapita ikiwa ni pamoja na mifugo na wanyamapori”alisema Mhina.

Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Endepesi,kijiji Cha kimokouwa Wilayani hapa,Losinyati Laizer aliishukuru Serikali kwa kuwapelekea mradi huu mkubwa wa maji na kwamba utakuwa ni mkombozi mkubwa sana kwao kukabiliana na changamoto ya upatikani wa maji ambayo wamekuwa nayo kwa muda mrefu.

Share To:

Post A Comment: