Kutoka katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tayari viongozi wa kiserikali na Chama cha Mapinduzi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani wameshaanza kuingia kwenye uwanja huu tayari kumuaga mpendwa wetu Dk John Magufuli.


Mageti ya uwanja wa CCM Kirumba yamefunguliwa toka saa 12 alfajiri na wananchi ni wengi sana ambao wako nje ya uwanja wakiendelea kuingia kwenye uwanja huu.

Mikoa zaidi ya mitano ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Tabora na Mara yote wananchi wake kwa uwingi wao wanaendelea kuingia kwenye uwanja huu.

Mwili wa aliyekua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli aliyefariki Machi 17 mwaka huu utaagwa kwenye uwanja huu kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Chato, Geita kwa ajili ya mazishi.









Viongozi mbalimbali wakijadiliana jambo mapema leo asubuhi ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba wakati wakisubiri kuwasili wa kwa Mwili wa Hayati Dkt Magufuli













 Wananchi wa Mwanza tayari wamewasili katika uwanja wa CCM Kirumba tayari kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Share To:

Post A Comment: