Mwenyekiti wa Soko la Kimataifa la Vitunguu Mkoa wa Singida, Idd Mwanja akizungumza na Wafanyabiashara wa zao hilo wakati akitoa  taarifa ya mapato ya mwaka jana kwenye mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa soko hilo uliofanyika jana.


Wafanyabiashara wa vitunguu wakiwa kwenye mkutano huo.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wakina mama wakichagua vitunguu kwenye soko hilo.
Mkutano ukiendelea.

Vitunguu vikiwa sokoni katika soko hilo. 


Na Ismail Luhamba,Singida.

WAFANYABIASHARA katika Soko la Kimataifa la Vitunguu lililopo  mkoani Singida walia na Serikali juu ya vipimo vya kufungasha bidhaa hiyo kwani havilingani na masoko mengine.

Wafanyabiashara hao waliyasema hayo  wakati wa ufunguzi rasmi wa Soko hilo msimu wa mwaka 2021 ambalo lilifunguliwa na Mwenyekiti wa soko hilo, Idd Mwanja.

Waliiomba Serikali kusaidia suala la vipimo ili viwe vinafanana ndani ya masoko yote hapa nchini kwani kuna masoko mengine wana vipimo tofauti jambo ambalo linawawia vigumu kufanya biashara hasa pale inapoonekana kipimo chako ni kidogo.

"Hatukatai hivi vifungashio na vipimo ila tunachoomba ni vifungashio kwa maana ya vipimo viwe vinafanana nchi nzima..ukipeleka vitunguu Dar es salaam unakutana na vipimo vingine kutoka maeneo mengine na ni kipimo kikubwa, hivyo vifungashio vyetu vinaonekana havifai."

Awali akifungua soko hilo Mwenyekiti wa soko,  Idd Mwanja alianza na kutoa taarifa ya mapato mwaka 2020 ambapo alisema jumla ya magunia ya vitunguu yaliyoingia sokoni hapo ni laki 103913 sawa na shilingi milioni 207,826,000 zilizotokana na ushukuru wa magunia hayo.

"Hii hesabu ni kwa kikundi kimoja tuu kilichokusanya ukiachilia mbali vikundi vingine vinavyoshughulika na magunia yanayobebwa na mikokoteni na gari zingine ndogo."

Licha ya Soko hilo kuiingizia Serikali kipato kikubwa kiasi hicho lakini bado miundombinu yake sio rafiki kwa wakulima na wafanyabiashara kwa ujumla ambapo mvua zikinyesha wakulima na wafanyabiashara wanalazimika kuuziana vitunguu uchochoroni kuepusha kuozesha mali zao jambo ambalo linapelekea Serikali kukosa mapato.

"Naiomba Serikali ya Manispaa ya Singida wafanye ukarabati wa haraka ili waendelee kupata mapato na kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara kunufaika na soko hili."

Akielezea dira na mpango mkakati wa msimu wa mwaka huu Mwanja alisisitiza na kuwataka wafanyabiashara kwenye soko hilo kufuata maelekezo ya suala la vipimo kwani uongozi umeelekeza gunia linatakiwa kushonwa ujazo usio zidi kilo 110.

Hata hivyo ameomba masoko mengine katika mikoa inayolima zao hilo kutumia vipimo hivyo ili kuwanufaisha wakulima, wafanyabiashara na Serikali kwa ujumla.

"Naomba mikoa mingine watuunge mkono katika hili,unakutana wafanyabiashara wengine wanapima vitunguu kwa kutumia ndoo na wanapima ndoo 10 ndani ya gunia moja hiyo ni kumnyanyasa mkulima." alisema Mwanja.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Khamis Kisuke aliwaambia wafanyabiashara hao kuwa Manispaa imetenga bilioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo pamoja na kutengwa fedha hiyo pia Manispaa imetenga milioni 14 kwa ajili ya matengenezo ya awali kabla ya kuanza ujenzi ambapo shughuli itaanza muda wowote kuanzia sasa.

Aidha aliwataka wafanyabiashara katika soko hilo kuwa waaminifu wanapofanya biashara zao na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu na kwamba mwenyezi Mungu ameagiza hayo hivyo tuyafuate ili tuje tuione akhera.
Share To:

Post A Comment: