Katibu Hamasa na Chipukizi Mkoa wa Arusha Edson Ndyemalila akihutubia wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (CDTI).


Vijana watakiwa kutumia ujana wao kuweza kutetea uhuru wa nchi yao ili baadae waweze kuweka historia kwa mambo ambayo watakuwa wameyafanya ndani ya Chama cha Mapinduzi kwani chama kina lenga kuwataka vijana kuwa na maadili katika jamii na sio kukaa na  kutumia mitandao ya kijamii katika kughushi habari za uongo kwa viongozi wa Serikali na ndani ya Chama.

Hayo yamesemwa na Katibu Hamasa na Chipukizi Mkoa wa Arusha Edson Ndyemalila  katika Darasa la Itikadi Uongozi na Uzalendo katika Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (CDTI) kwa lengo la kuwapa uelewa wa chama cha Mapinduzi na taratibu zake kwa ujumla ambapo amesema kuwa kusoma na elimu wanayopatiwa vijana hao kutawaongezea maarifa ya kupata ufahamu wa taarifa mbalimbali zinazohusu chama na serikali.

Pia amewataka vijana hao kuendelea kujenga tabia ya kuwekeza michango yao katika jamii kabla ya kuwa kiongozi ili kuweza kushawishi watu watakaowaongoza na wasisubirie kuwa kiongozi ndio watoe michango yao kwani watakuwa wanaharibu mwonekano na taswira ya kuwa kiongozi kwa watu wtakaowaongoza.

Aidha amewataka wanafunzi hao kuwa wazalendo katika kutatua changamoto katika jamii inayowazunguka na kutosubiri hadi wawe viongozi ndio wafanye hayo kwani watakuwa wanajipunguzia sifa ya kuwaongoza wananchi na kushindwa kuchaguliwa kwa kukosa sifa ya utumishi kabla ya kuhitaji uongozi.

“Uzalendo unamiiko yake, kwamba mtu mzalendo ni mstaharabu na awezi kufanya mambo ambayo wenzake wanachukia lakini wengine wanapoambiwa sio mstaharabu maana ustaharabu kauponyoka, hawaheshimu watu,vitu na hata rasilimali za jumla haziheshimu"  Ndyemalila

"Lazima vijana muwe mumejiandaa katika utumishi na uongozi  kwa jamii nakuleta maendeleo kabla ya kugombea ili kuweza kuwashawishi watu mtakaowaongoza katika jamii inayokuzunguka hii ni moja ya sifa itakayowasaidia kuwa kiongozi kwa wananchi na kuweza kukuamini kukuchagua" Ndyemalila

Pamoja na hayo Edson Ndyemalila amewasisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi kina lenga kuwataka vijana kuwa na maadili na kutumia mitandao ya kijamii katika kujenga Chama na sio kutumia kughushi habari za uongo kwa viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi.

Kwa Upande wake Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM) wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Arusha Wema David Somba amewataka wanavyuo hao kuhakikisha wanatumia fursa wanayoipata kwa maslahi ya wananchi pia wawapuuze watu wachache wanaoharibu sifa ya chama hicho.

Wema amewataka  vijana hao wakawe chachu kwa Chama cha Mapinduzi katika Mkoa wa Arusha ili kumuenzi Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri alizofanya za kimaendeleo tokea kuchaguliwa kwake.

Wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru wakifuatilia mdahalo.




Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM) wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Arusha Wema David Somba akizungumza na Wanafunzi.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinzuzi UVCCM Mkoa wa Arusha John Nkini akitoa ssemina kwa Wanafunzi wa CDTI Tengeru
Share To:

Post A Comment: