Na Woinde Shiza ,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Hassan Kimanta ameridhishwa na namna ujenzi wa majengo ya afya na shule katika wilaya ya Longido unavyoendelea.
Kimanta ameyasema hayo alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo na kuwapongeza kwa juhudi walizozifanya katika usimamizi.
Aidha, Kimanta ametoa wito kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha watumie wajenzi wa kawaida katika kujenga miundombinu ya maendeleo hasa pale inapotakiwa kufanya hivyo ili kupunguza gharama za ujenzi.
Amewasisitiza kuendelea kusimamia miradi hiyo kwani serikali inatoa fedha nyingi ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Nae, Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisombe amesema wilaya itaendelea kusimamia miradi kwa ukaribu zaidi ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Post A Comment: