Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam.
Waziri mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Sadick Meck Sadick akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Mbatilo)
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wadau wa sekta ya Uvuvi nchini wametakiwa kutumia fursa zinapojitokeza katika sekta hiyo ili kuweza kukuza uchumi wakati huo huo wakihakikisha wanatokomeza uvuvi haramu.
Ameyasema hayo jana Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul alipokuwa anafunga Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Uvuvi nchini uliofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati anafunga mkutano huo Mhe.Gekul alisema kupitia mkutano wa wadau wa uvuvi wameweza kuibua fursa mbalimbali zinazohusiana na Uvuvi hivyo wadau wakitumia vizuri fursa hizo wanaweza kunufaika.
"Moja ya fursa ambayo wameza kuibua ni pamoja na uwekezaji katika bahari kuu, tumeona TAFICO inavyokwenda kufufuliwa pamoja na ujenzi wa bandari ya Uvuvi Mbigani Bagamoyo pamoja na kununua meli 4 na kwa ujumla zinakuwa 8 na Zanzibar kwaajili ya kuanza uwekezaji katika bahari kuu". Alisema Mhe.Gekul.
Aidha Mhe.Gekul alisema wameweza kufahamu mahitaji ya vyakula vya samaki kwamba nikiasi gani wajiandae kuelekea kwenye kilimo cha ufugaji wa samaki katika mizimba pamoja na mabwawa.
"Tunapoelekea kukuza sekta ya uvuvi ni vizuri tukatumia fursa ya upatikanaji wa dhana bora ya uvuvi ili kuweza kuwanufaisha wavuvi pamoja na wananchi kwa ujumla na kuweza kukuza uchumi". Alisema.
kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizaya Viwanda na Biashara amesema kuwa katika wiki mbili zilizopita kulitokea taarifa ya samaki kuonekana wamekufa katika maeneo mbalimbali ya ziwa Victoria na kuwapa watu hofu ya uwezekano wa samaki wale kuwa na sumu, hivyo kukatumwa timu ya maabara kwaajili ya kujiridhisha na majibu yalivyotoka ikaonekana kuwa hawakuwa na sumu.
"Baada ya hofu kutokea nilituma timu yangu ya maabara na kuchukua sampo ya samaki katika maeneo ya Rorya, Musoma, Mwanza,Sengerema na Bukoba tukazipeleka kwa mkemia mkuu ili aweze kuangalia kama kuna sumu au wamekufa kwa mabadiliko ya tabia nchi".
Amesema matokeo yalivyotoka na kuonesha kwamba sampo zote za samaki walizopeleka hakuna samaki yoyote aliyekutwa na sumu.
" Kuna hali huwa inajitokeza ziwani kwenye miezi ya baridi ambayo inafanya maji ya juu kupata baridi na kuwa nyuzi joto sawa na yale ya chini hivyo ikitokea upepo maji ya chini yanakuja juu na kuchanganyikana na kusababisha baadhi ya samaki kufa". Amesema
Post A Comment: