Mkurugenzi
Mkuu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia
Generali John Mbungo amesema wamefanikiwa kutekeleza mapambano dhidi ya
rushwa kwa 89.8% kwa mwaka 2019/2020 tofauti na mwaka 2018/2019 ambapo
walifikia 88.1%.
Mbungo amebainisha hayo wakati akikabidhi ripoti
yake kwa Rais, Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Chamwino Jijini
Dodoma mapema hii leo.
Amesema mafanikio hayo yamekuja kutokana
na kutoa elimu kwa umma kuhusiana na madhara ya rushwa kwa wananchi
ambapo semina zipatazo 3683 zilitolewa na kusaidia majalada 1079
kukamilika tofauti na mwaka uliopita ambapo yalikuwa 911.
“Kati
ya majalada hayo majalada 385 yalihusu hongo na majalada mengine 694
yalihusu vifungu vingine vya sheria vya kuzuia na kupambana na rushwa”
amesema Mbungo.
Aidha, amebainisha kuwa hadi majalada hayo
uchunguzi wake unakamilika uligusa sehemu mbalimbali ikiwemo ukiukwaji
wa sheria ya manunuzi ya umma, vyama vya ushirika vya masoko ya mazao
ya kilimo kutowalipa wakulima baada ya kuuza mazao yao kwenye vyama
hivyo, mikopo umiza na ufujaji wa fedha katika miradi ya maendeleo.
Post A Comment: