Mkuu wa TAKUKURU-ARUMERU Bwana Deo Mtui (kushoto) akikabidhi kiasi cha Tshs.7,000,000/= kwa maafisa mapato wa Halmashauri ya Meru kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya MERU.
Na Kiasi cha Tshs.300,000/= ni fedha za Mwananchi Mnyonge aitwaye Anate Nanyaro ambaye alikuwa amedhulumiwa na Mwajiri wake kiasi cha Tshs.1,000,000/=
Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya ARUMERU Ndg. Deo Mtui amesema fedha hizo za USHURU wa Usafi na Mazingira, kiasi cha Tshs.19,500,000/=
zimetolewa kwa awamu nne (4)
ambazo zilikabidhiwa kwa maafisa mapato wa Halmashauri ya MERU, Emiliana Julias, Neema Mollel, Sigfrid Janga na Mabuye kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Ndugu EMMANUELI MCONGO.
Ambapo, awamu ya kwanza tarehe 28/02/2021 kilikabidhiwa kiasi cha Tshs 7,000,000/=, awamu ya pili, Tarehe 03/03/2021, kiasi cha Tshs.6,000,000/=, kiasi kingine cha Tshs.5,200,000/= kilikabidhiwa tarehe 09/03/2021 na awamu ya nne, kilikabidhiwa tarehe 12/03/2021 kiasi cha Tshs.1,300,000/=, sambamba na fedha kiasi cha Tshs 300,000/= alizodhulumiwa mwananchi mnyonge aliyekuwa na shida ya haraka ya kutatua.
Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya ARUMERU, Bwana Deo Mtui amesema TAKUKURU Wilayani Arumeru imejipanga kuhakikisha Wananchi wote waliodhulumiwa ndani ya wilaya ya ARUMERU kwa namna yoyote ile wanapata haki yao kwa wakati sambamba na kudhibiti ubadhirifu na ufujaji wa fedha za umma kwa uthubutu wa kutokumvumilia mtu yeyote.
Mtui ametoa wito huo kwa Wananchi wote waliodhulumiwa haki zao na ambao wameshindwa kuzipata haki hizo kwa wakati wasisite kufika TAKUKURU ARUMERU na kwenye ofisi mbalimbali za TAKUKURU nchi nzima ili wapatiwe haki zao.
Post A Comment: