Na,Jusline Marco;Arusha
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Dkt.Faustine Ndugulile amelipongeza shirika la posta mkoa wa Arusha kwa juhudi za uongezaji wa mapato ya shirika na kufikia hatua nzuri ya malengo ambayo yanakusudiwa na kulitaka shirika hilo kuendana na mazingira ya aasa ya kidigitali.
Akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea taasisi zinazohusika na wizara hiyo Mhe.Ndugulile amesema kuwa lazima kuwepo na malengo ya taasisi,mkoa,kitengo na ya mtu mmojammoja kwani kila kitu sasa hivi kinafanyika katika mifumo ya kidigitali
"Nimeangalia masanduku pale nimeona zaidi ya asilimia 70 hawaji hata kuchukuwa barua zao,hawazihitaji kwahiyo biashara sasa hivi kuwa na masanduku hayana tija,dunia ilishahama hivyo lazima shirika la posta liendane katika mazingira ta sasa."alisisitiza Waziri Ndugulile
Aidha amesema kuwa ni vizuri kama shirika na kama watumishi wakajipanga wenyewe kwa kuleta posta mpya yenye utendaji na matokeo mapya katika uletaji wa malengo ya shirika amnapo amelitaka shirika la hilo kuhakikisha kuwa hadi ifikapo tarehe moja Juni wawe wameboresha mfumo wa uendeshaji wa huduma za posta.
Awali akizungumza na uongozi na mamlaka ya mawasiliano Tanzania,TCRA Mkoa wa Arusha ameiagiza mamlaka hiyo kuelekeza nguvu kubwa ya kutoa elimu kwa jamii dhidi ya matumizi sahihi ya mitandao.
Nae mkuu wa mamlaka hiyo Kanda ya kaskazini Imelda Salum akitoa taarifa ya mamlaka kwa waziri amesema kuwa wamekuwa wakielimisha wananchi kutambua wajibu na haki zao, usajili wa line kwa alama za vidole na urasimishaji wa line za simu.
Akisoma taarifa ya utendaji katika Mikoa ya Arusha na Manyara,Meneja Posta Mkoa wa Arusha Athman Msilikile amesema katika miradi mipya ya kimkakati Mkoa wa Arusha na Manyara,mradi wa usafirishaji Sampuli unaofanyika katika Wilaya 13 kwenye Mkoa wa Manyara na Arusha inahusisha 'Hub'19 na 'Spokes'zaidi ya 303 ambapo mradi huo ulianza mwezi februari mwaka huu kwa kushirikiana na NGO ijulikanayo kama EGPAF na unatarajiwa kuzalishwa 600M kwa mwaka.
Ameongeza kuwa kwa mwaka shirika linatarajia kupata shilingi milioni 40 kupitia upangishaji wa plots katika majengo ya Babati Mkoani Manyara hulu katika uzalishaji wa kituo cha kuuza na kununua hisa pamoja na hati fungani kwa shirika na soko la hisa la DSM(DSE) na mkoani Arusha HPO utakuwasehemu ya mradi wa 'One Stop Centre'.
Msilikile ameeleza kuwa hali ya utoaji wa huduma kwa mkopo na ukusanyaji wa madeni mkoani Arusha kwa kipindi cha mwezi jilai hadi mwezi Desemba mwaka jana ulikuwa asilimia 76 na kusema kuwa mkoa unafanya juhudi za makusudi ili kuongeza kasi ya makusanyo ya madeni ambapo kamati ya madeni imeimarishwa kwa kufuatilia wadaiwa wote.
Vilevile amesema kuwa shirika linamiliki viwanja 19 kati ya hivyo 17 hati miliki zimekamilika huku kiwanja kimoja kikiwa katika hatua ya kupatiwa hati na kimoja kikiwa katika hatua za ufuatiliaji ambapo katika viwanja hivyo mkoa umefanya uwekezaji kwa kupangisha majengo na na viwanja vya wazi kwa lengo la kukuza mapato ambapo mkoa umeweza kuingia mikataba 43 na wawekezaji yenye thamani ya zaidi ya shilingi molioni 20 kwa mezi na zaidi ya shilingi milioni 240 kwa mwaka.
Pamoja na hayo amebainisha changamoto za kibiashara katika mkoa wa Arusha kuwa ni uchakavu wa majengo ya shirika kwa ajili ya ofisi na makazi ya kupangusha hali iliyopelekea wapangaji kulipa kodi kwa malalamiko.
Katika Mkoa wa Manyara Msilikile ameeleza kuwa katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana jumla ya masanduku 15325 yalisimikwa na masandjku 14730 yalikodishwa huku masanduku 7940 yalilipiwa hivyo kupelekea mkoa kukusana mapato ya masandjku yaliyosimikwa kwa asolkmia 51.8
Sambamba na hayo ameongeza kuwa kwa kipindi hicho mapato ya mkoa huo yalishuka kwa asilimia 23.3 ikilinganishwa na kipindi cha mwezi jilai hadi Desemba 2019 kwa sababu ya biashara ya utalii kushuka hivyo kuathiri mapato ya mkoa huo.
Post A Comment: