RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu ameongoza maelfu ya wananchi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt.John Magufuli ambaye ameagwa leo Machi 20,2021 katika Uwanja wa Uhuru.
Dk.Magufuli alifariki dunia Machi 17,2021 katika Hospitali ya Mzena Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo na leo kwa mujibu wa ratiba wananchi wa mkoa huo wakiongzwa na Rais Mama Samia wametoa heshima za mwisho kwa mwanamapinduzi na mpenda maendeleo wa Taifa la Tanzania.
Kabla ya Rais Mama Samia kuongoza kutoa heshima za mwisho ilifanyika Misa maalum katioa Uwanja huo wa Uhuru iliyoanza baada ya mwili kuwasili saa 10:13 asubuhi ukitokea Kanisa la mtakatifu Petro (St.Peters') ambako nako ilifanyika Misa ya wafu.
Baada ya Rais Samia kutoa heshima zake kwa Dkt.Magufuli alifuata Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aiyekuwa amefuatana na mkewe na baada ya Waziri Mkuu kutoa heshima zake aliondoka uwanjani hapo.Wengine walitoa heshima ni Mama Maria Nyerere,akifuatiwa na Mama Janeth Magufuli aliyeongozona na familia yake.
Viongozi wengine ambao waliotoa heshima za mwisho ni Katibu Mkuu kiongozi Dkt. Bashiru Ally Kakulwa. Rais mstaafu Aman Abedi Karume, majaji wastaafu wakiwamo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalaama.Pia viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo Mawaziri pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Baada ya hapo wakafuata wananchi waliokuwa wamesimama katika misururu mirefu.
Awali wakati akiongoza Misa katika Uwanja huo, Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam Tadeus Rweich amewaomba watanzania waliojitokeza viwanjani hapo na waliotazama kupitia televisheni zao majumbani, amumelezea Hayati Dkt. Magufuli ambapo amesema alikuwa ni Rais aliyeipenda nchi yake na alifanya kazi zake Kwa uzalendo mkubwa na Kwa nguvu zake zote.
Amesema Dkt.Magufuli alikuwa ni mtu wa Mungu kweli kwani kila alichokifanya kwake Mungu alikuwa mbele, alijali maslahi ya Taifa na aliwapenda Watanzania kwa vitendo.
Aidha Askofu Rwaich ametoa pole Kwa Rais Mama Samia pamoja na familia ya Hayati Dkt.Magufuli Mama Janeth Magufuli katika kipindi hiki kigumu kuwa mstamilivu na kushikamana na Mungu na kubwa zaidi kumuombea.
Pia ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa Watanzania wote na kuwataka kujipa moyo na matumaini na kwamba yeye hana shaka kwamba Rais Samia atatenda vyema, haki katika shughuli zake mpya majukumu yake.
Post A Comment: