Rais
wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko,
kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha bandarini.
Rais Samia
amefikia uamuzi huo leo Jumapili, Machi 28, 2021 baada ya ripoti ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru Ikulu
ya Chamwino, Dodoma.
“Ripoti nimeona, nimeipitia na nimebaini
ubadhirifu mkubwa uliofanywa pale bandari, hili suala mnatakiwa
kushirikiana, nakuomba Takukuru jishughulishe pale, alipita Waziri Mkuu
alilishughulikia.
“Waziri Mkuu aliunda kamati na wakafanya
uchunguzi kidogo ambao yaliyotoka, hatua chache zilichukuliwa lakini
imani yangu ni kwamba kama kuna ubadhirifu pale waliosimamishwa ni hawa
wa chini huku, ninaomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi
Mkuu wa Bandari halafu hatua zaidi ziendelee,” amesema Rais Samia.
Post A Comment: