Teddy Kilanga


Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt.John Pima amekabidhi mipira mitano mwenyekiti wa timu Arusha FC kama sehemu ya mchango wa almashauri hiyo ili kusukuma mbele timu hiyo na kuweza kufikia nafasi nzuri katika michuano yake.


Akikabidhi mipira hiyo, Mkurugenzi Pima amesema kuwa mbali na utoaji wa mipira hiyo wanampango wa kusaidia timu hiyo ili iweze kufika sehemu nzuri ikiwa kwa sasa ipo daraja la 1 .


Aidha Dkt Pima amewaba wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo ili kuhakikisha wanapata vifaa ambavyo vitawasaidia katika kabumbu, na kusonga mbele zaidi lengo likiwa ni kutambulisha jiji kwani huo ni mwendelezo wa juhudi  mh.Rais wa jamuhuri wa Tanzania.


Nae mwenyekiti wa Arusha Football Club Elly Kisanga  amemshukuru Mkurugenzi kwa kuwapatia mipira hiyo na muahidi ushindi katika mechi wanayotarajia kucheza juma mosii ya wiki hii kwani hapo awali walikuwa na mipira miwili tu,na kuwaomba wadau wengine kuunga mkono jitihada za Mkurugenzi ikiwa tawi la Yanga Mkoani hapa limeshatoa mpira 1.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: