Mwili wa mfanyabiashara maarufu,Andrew Mollel aliyafariki hivi karibuni jijini Arusha unatarajiwa kuzikwa March 3 mwaka huu katika makaburi ya familia yaliyopo kata ya Olorien mkabala na ofisi za TBC jijini hapa.
Mollel,ambaye alikuwa mkurugenzi wa kampuni mbalimbali ambazo ni Happy Sausages, Kijenge Animal Products Ltd na mvumbuzi wa mchoro wa nyumba za PPF KIjenge anatarajiwa kuzikwa na wafanyabiashara,wanasiasa pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini.
Akihojiwa na waandishi wa habari nyumbani kwake Leo ,mtoto wa marehemu ,Derrick Mollel alisema kwamba mwili wa marehemu baba yake unatarajiwa kuagwa katika katika kanisa la KKKT Mjini Kati majira ya saa sita mchana na kisha kwenda kupumzishwa katika makaburi ya familia yaliyopo Olorieni mkabala na ofisi za TBC jijini Arusha.
Baadhi ya wafanyabiashara pamoja na wanasiasa mbalimbali hapa nchini akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa CCM ,Comrade Abdulraham Kinana wamefika nyumbani kwa marehemu Leo kutoa pole kwa familia.
Mwisho.
Post A Comment: