Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma Dkt. Momole Kasambala akizungumza katika Kikao cha Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kilichofanyika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA) mkoani Morogoro leo Machi 29, 2021.
Mwakilishi wa Meneja Rasilimali Watu TIA, John Gama, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake (RAAWU), TIA, Kampasi ya Singida, Seba Ernest, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa kikao hicho, Alton Kanjolonga kutoka Kampasi ya Singida, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Wajumbe wa baraza hilo wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Wajumbe wa baraza hilo wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MAFUNZO kwa njia ya mtandao ambayo yanatarajiwa kutolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yatawanufaisha wananchi wengi.
Hayo yamebainika katika Kikao cha Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi wa TIA kilichofanyika jana Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA) mkoani Morogoro.
Wajumbe wote kabla ya kuanza kikao hicho walisimama kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza katika kikao hicho Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma Dkt. Momole Kasambala alisema mafunzo hayo yanatarajia kuanza pindi utakapo kamilika utafiti wao na kuwa yatatoa fursa kwa wananchi wengi kuyapata.
"Tupo kwenye mchakato wa kuanza kutoa mafunzo haya na tukisha kamilisha kufanya utafiti wetu tutaanza kuyatoa wakati wowote." alisema Kasambala.
Kasambala akizungumzia mahusiano ya chuo hicho na vyuo vingine alisema kitaanzisha mahusiano na
ushirikiano na vyuo vya ndani na nje ili kubadilishana uzoezi wa ufundishaji.
" Hivi sasa tunaandaa maridhiano ya pamoja baina yetu na Chuo Kikuu cha Irkutsk cha Urusi ili kuanzisha ushirikiano huo." alisema Kasambala.
Alisema katika kikao chao cha maazimio cha mwaka jana waliazimia kuingia mikataba na baadhi ya taasisi za kifedha kama benki ya Posta, CRDB na NMB kwa ajili ya kuwakopesha wafanyakazi wao riba nafuu ambapo tayari Benki ya NMB imefanya mkataba nao ambapo riba yao ni 15%.
Post A Comment: