Wananchi wa eneo la Kinondoni B na Biafra wakiwa kandokando ya barabara kwaajili ya kuaga mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 20, 2021.
MAELFU ya wananchi wa Mkoa Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kwenye barabara ambayo mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli unapitishwa ukitokea Kanisa la St.Peters kuelekea Uwanja wa Uhuru.
Wananchi hao walianza kujitokeza mapema ya alfajiri katika barabara ya Moroco,Magomeni,Ilala Boma,Chang'ombe , Chuo Kikuu cha Ualimu Dar es Salaam( DUCE) hadi Uwanja wa Uhuru.
Barabarani watu waliokuwa wamejazana kushuhudia jeneza la mpendwa wetu Dk.Magufuli,wengi wao walishindwa kujizua. A kijikuta wakiangaua vilio ,wengine wakionekana wako chini kutokana na kuishiwa nguvu.
Hakika ni majonzi na simanzi kubwa iliyokuwa imetawala .Mwili wa Dk.Magufuli ulianza kupitishwa barabarani kuanzia saa tatu baada ya kumalzika kwa ibada maalum iliyofanyika Kansa la St.Peters mkoani Dar es Salaam.
Kadri mwili ulivyokuwa unapita barabarani ndivyo ambavyo idadi ya wananchi ilivyokuwa ikiongezeka ili.kushuhudia mwili wa Dk.Magufuli ukpitishwa.Wananchi waliokuwa barabarani mbali ya kuangua vilio na kujawa na simanzi , wengine walikuwa wameshika majani ya matawi ya miti
Michuzi TV na Michuzi Blog imeshudia pia idadi kubwa ya wanafunzi katika eneo la Kinondoni Biafra ambao nao waliamua kujitokeza kumuaga Dk.Magufuli ambao nao walishindwa kujizuia,walikuwa wanalia muda wote wakati mwili unapitishwa.
Ku to kana na msiba huo.mkubwa ambao Taifa la Tanzania imeupata, barabarani ambako mwili ulikuwa unapitishwa hakukua na shughuli nyingine zozote zaidi ya wananchi maelfu kwa maelfu mujipanga barabarani.Endelea kufuatilia Michuzi TV na.Michuzi Blog kwa taarifa zaidi.
Post A Comment: